Habari za Punde

Walimu Wilaya ya Kusinin Unguja Kusimamia Miungozo na Taratibu Zilizowekwa na Wizara ya Elimu.

Na.Takdir Suweid. Maelezo Zanzibar.
Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya ya Kusini Kassim Abuu Mtoro amewataka Waalimu wakuu kusimamia miongozo na taratibu zilizowekwa na Wizara ya elimu ili kuondosha matokeo mabaya katika Wilaya hiyo.

Ameyasema hayo huko Skuli ya Kitogani wakati alipokuwa katika kikao cha kujadili maendeleo ya elimu katika Halmashauri hiyo.

Mtoro amesema Halmashauri haitosita kuwachukulia hatua Waalimu watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Hata hivyo amewataka Waalimu kusomesha kwa kutumia mbinu bora na  za kisasa na badala yake waache kusomesha kwa mazoea.

Mbali na hayo amemuagiza Naibu Mkurugenzi elimu Halmashauri ya Wilaya ya Kusini kuweka utaratibu wa kupita kila shehia kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa elimu kwa Watoto wao.

Kwa upande wake Afisa elimu Wilaya ya Kusini Hamid Abdul-hamid Khamis amesema ufaulu hauridhishi hasa kwa Skuli za Maandalizi na Msingi kutokana na mashirikiano madogo kwa ya baadhi ya Wazazi na Waalimu,Uwajibikaji mdogo wa Waalimu wakuu na juhudi ndogo ya Wanafunzi katika kudurusu masomo.

Nao baadhi ya Waalimu hao wamesema suala la kuwafanya Wanafunzi kufaulu vizuri linahitaji mashirikiano lakini cha kusikitisha ni kupewa lawama Waalimu pekee Wakati wanafunzi wanapofanya vibaya jambo ambalo jambo ambalo linaweza kuwakatisha tama na kuwarudisha nyuma.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.