Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Mussa Azzan Zungu akikaribishwa rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Jijini Dodoma.
Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Joseph
Malongo na Balozi Joseph Sokoine Naibu Katibu Mkuu.
Na
Lulu Mussa
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu amemtaka kila
mtumishi katika Ofisi ya Makamu wa Rais atimize wajibu wake katika kuleta
maendeleo ya Taifa letu.
Hayo ameyasema hii leo mara
baada ya kuwasili rasmi katika Ofisi ya Makamu wa Rais katika Mji wa Serikali
Mtumba Dodoma na kupokewa na Menejimenti na watumishi na Ofisi hiyo.
Akizungumza na watumishi wa
Ofisi yake Waziri Zungu amewataka wote kufanya kazi kwa ushirikiano na kuahidi
kuendelea kusimamia Sheria, Taratibu na Kanuni zilizopo.
Ametoa rai kwa watanzania
kuwa chachu ya mabadiliko katika kuhifadhi na kusimamia Mazingira. “Simamieni
Sheria bila kumuonea mtu, pale ambapo Sheria imekataza jambo simamieni Sheria
na kuchukua hatua kwa wote wanaokiuka” Zungu alisisitiza.
Awali aliyekuwa Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) ambae sasa ni wa Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. George Simbachawene amekabidhi Ofisi rasmi kwa
Waziri Zungu na kumtakia kila la heri katika kutekeleza majukumu yake mapya.
“Tumefanikiwa katika katazo
la mifuko ya plastiki, tumeridhia Mikataba na Itifaki mbalimbali na pia tuna
program maalumu ya Upandaji mti nchi nzima ambayo ni endelevu” Simbachawene
alisisitiza.
Pia Mhe. Waziri Simbachawene
alisema kuwa mbali ya kufanikiwa katika kampeni ya katazo la mifuko ya plastiki
lakini zaidi na elimu inapaswa kutolewa kwa wananchi kuhusu tofauti ya
vifungushio na vibebeo ambavyo bado wananchi wanachanganya.
Amempongeza na kumshukuru
Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Mhandisi Joseph Malongo kwa muda aliofanya nae kazi
kwa ukaribu ambapo wameweza kutekeleza majukumu mbalimbali yakiwemo kuridhia
mikataba, itifaki na kanuni zinazohusu mazingira.
Waziri Zungu ameteuliwa hivi
karibuni na Rais Dkt. John Magufuli kushika nafasi hiyo baada ya kufanya
mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo Mhe. Simbachawene aliteuliwa
kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Mussa Azzan Zungu akiongea na Menejimenti ya Ofisi yake mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo katika Mji wa Serikali wa Mtumba mapema leo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe.
Mussa Azzan Zungu akiongea na sehemu ya watumishi wa Ofisi yake mara baada ya kuwasili katika Ofisi hiyo katika Mji wa Serikali Mtumba mapema leo.
Pamoja na mambo mengine amewasisitiza watumishi hao kufanyakazi kwa uadilifu kwa kuzingatia Sheria,
Kanuni na taratibu zilizopo.
Aliyekuwa
Waziri waNchiOfisiyaMakamuwaRaisambaesasani Waziri wa Mambo yaNdaniyaNchiMhe.
George SimbachaweneakimkabidhirasmiOfisi Waziri waNchiOfisiyaMakamuwaRais
(MuunganonaMazingira) Mhe. MussaAzzanZungu.
MakabidhianohayoyamefanyikahiileokatikaMjiwaSerikaliMtumba – Dodoma.
Waziri
waNchiOfisiyaMakamuwaRais (MuunganonaMazingira) akiwana Waziri wa Mambo
yaNdaniyaNchiMhe. George SimbachawenemarabaadayakukabidhianaOfisihiileoMtumba
Dodoma. WenginekatikapichaniKatibuMkuuOfisiyaMakamuwaRaisMhandisi Joseph
Malongo, NaibuKatibuMkuuBalozi Joseph SokoinenaMkurugenziMkuuwaBaraza la Taifa
la HifadhinaUsimamiziwaMazingiranchini (NEMC) Dkt. SamwelMafwenga.
No comments:
Post a Comment