Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu.Mhe. Jenista Mhagama Arizishwa na Ujenzi wa Jengo la NEC Dodoma.

Muonekano wa sehemu ya jengo la Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliyopo eneo la Njedengwa Jijini Dodoma.

Na.Mwandishi Wetu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ametembelea na kukagua hatua ya ujenzi wa jengo la Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi zilizopo eneo la Njedenwa Jijini Dodoma na kusema ameridhishwa na hatua iliyofikiwa.
Alikagua mradi huo, Januari 07, 2020 ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoyatoa Novemba 18, 2019 alipotembelea na kukagua mradi huo na kutoridhishwa na kasi ya ujenzi na kutoa maagizo hayo baada ya TBA kusimamisha zoezi la ujenzi kwa ongezeko la gharama za  kutoka bilioni 13 hadi bilioni  32 na hivyo kumtaka Waziri Mhagama kufuatilia.
Ziara ya Waziri Mhagama imebaini maendeleo mazuri ya ujenzi na kufikia hatua ya asilimia 75 baada ya Tume hiyo kuingia mkataba SUMA JKT kuwapongeza wakandarasi kwa hatua hiyo wanayoendelea nayo.
“Kwa kipindi chote ambacho SUMA JKT imeendeela na kazi ya ujenzi wa jengo hili hali inaridhisha na ni vyema kuhakikisha mnaendana na kasi inayotakiwa kwa kuzingatia gharama zilizokubalika za bilioni 16,”Alisistiza Waziri Mhagama
Alieleza kuwa ujenzi wa majengo ya Serikali ni moja ya hatua za kuhakikisha zoezi la kuhamisha watumishi Dodoma linafanikiwa kwa kuendelea kuweka miundombinu rafiki ya ofisi zao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama pamoja na Kanali Mabele ambaye ni Msimamizi mkuu wa mradi huo kutoka SUMA JKT wakiangalia sehemu ya majengo ya Ofisi  za Tume ya Uchaguzi yanayoendelea kujengwa  Jijini Dodoma wakati wa ziara yake katika mradi huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiweka saini katika kitabu cha wageni alipotembelea majengo hayo.
Mhandisi Michael Mussa akimuonesha Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama namna ujenzi unavyoendeelea katika miradi inayosimamiwa na Ofisi yake ikiwemo majengo ya Serikali Jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha watumishi wanakuwa na mazingira mazuri ya utendaji kazi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikagua ujenzi wa Majengo ya Ofisi ya Tume ya Uchaguzi yaliyopo Jijini Dodoma alipotembelea kujinea namna hatua hizo zinavyoendelea.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu )

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.