Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama katika kikao kazi, kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo leo. Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Mhe. Emmanuel Luhahula na Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama, Bi. Elizabeth Rwegasira (kushoto).
Mbunge wa Jimbo la Mkalama, Mhe. Allan Kiula akiwasilisha hoja za watumishi wa jimbo lake wakati wa kikao kazi kati ya Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama kilichofanyika leo katika ukumbu wa halmashauri hiyo.
Baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama wakimsikiliza Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) katika kikao kazi kilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo
Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa (Mb) amemuagiza Mkuu wa TAKUKURU Wilaya ya
Mkalama kuchunguza utendaji wa Kitengo cha Manunuzi cha Wilaya hiyo kutokana na
utekelezaji mbovu wa miradi ya maendeleo.
Agizo hilo amelitoa leo wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Mkalamakilichofanyika katika ukumbi wa halmashauri hiyo.
“Nataka TAKUKURU mkichunguze Kitengo cha Manunuzi cha Wilaya ya Mkalama kwa
sababu nimebaini kuna mwenendo mbaya katika utekelezaji wa miradi hapa wilayani”
Dkt. Mwanjelwa amesema.
Amefafanua kuwaKitengo hicho kimekuwa kikitoa tenda za miradi mbalimbali bila
kufuata utaratibu ikijumuishapia upotevu wa vifaa vya ujenzi katika mazingira
ya kutatanisha.
Dkt. Mwanjelwa ameweka bayana kuwa Serikali ya Awamu ya Tano imekuwa
ikijitahidi kuhakikisha inafikisha huduma karibu na wananchi akitolea mfano
ujenzi wa hospitali, upanuzi wa vituo vya afya na ujenzi wa masoko, lakini wako
baadhi ya watumishi wanaofanya ubadhirifu.
“Natoa onyo kwa watumishi ambao bado wanafikiria kujipatia fedha kupitia
miradi hii na ninawapa pole kwa sababu Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa
na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli haitaki mzaha katika utendaji kazi ”Dkt.
Mwanjelwa ameongeza.
Amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inataka watumishi walio safi
kiutendaji, wanaowajibika ipasavyo na wanaofanya kazi kwa kufuata kanuni na
taratibu za kiutumishi.
Katika hatua nyingine, Dkt. Mwanjelwa amemuelekeza Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Mkalama kutekeleza agizo laserikali la kuwaondoa kazini watumishi
wenye vyeti vya kughushi.
Maelekezo hayo ameyatoa baada ya kupokea malalamiko ya Mwalimu Mkuu wa
Shule ya Msingi Malela, Bw. Alfred Panda aliyetaka kujua hatima ya mmoja wa walimu
wake aliyebainika kuwa na cheti cha kughushiwakati wa zoezi la kusafisha
taarifa za watumishi, lakini amekuwa akiendelea na kazi na amefuatilia barua yake
ya kusimamishwa kazi bila mafanikio.
Dkt. Mwanjelwa amemtaka Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya ya Mkalama kulifanyia
kazi suala la mtumishi huyo haraka iwezekanavyo.
“Mkurugenzi hakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa haraka kwa mtumishi
huyu ambaye ana vyeti feki na unipe mrejesho” Dkt. Mwanjelwa amesisitiza.
Mhe.Dkt. Mwanjelwa yupo Mkoani Singida katika ziara ya kikazi yenye lengo
la kukagua utekelezaji wa shughuli za TASAFpamoja na kukutana na Watumishi,
kusikiliza maoni kero zao na kuzitatua.
No comments:
Post a Comment