04/02/2020
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu
waandishi wa Habari,
Nimekuwa nikipokea simu nyingi kutoka
kwa watu mbalimbali wakiuliza maendeleo ya
uchunguzi wa tukio la watanzania wenzetu 20 waliopoteza maisha huko
Mkoani Kilimanjaro baada ya kukanyagana kwenye hitimisho la kongamano la ibada
ya maombi tarehe 01.02.2020 na hatma ya
waliokuwa wakishikiliwa na Jeshi la polisi.
Kama ilivyokwisha kuelezwa na viongozi
mbalimbali na kwenye taarifa yangu kwenu ya tarehe 03.02.2020 hatua mbalimbali
zinazoendelea kuchukuliwa ni kwamba baada ya tukio hilo Mkuu wa Jeshi la Polisi
Tanzania Simon Nyakoro Sirro (IGP) alituma timu ya maofisa wakiwepo wataalamu
wa Uchunguzi wa Sayansi ya Jinai kwenda kuungana na timu ya wataalamu kule
Kilimanjaro katika uchunguzi.
Ndugu
waandishi wa habari,
Katika uchunguzi huo walikamatwa watu
nane (8) akiwepo Bonifase Mwamposa na kuhojiwa kwa kina na baada ya kujiridhisha
na yale yaliyokuwa yanahitajika kutoka kwao wamepewa dhamana kwa mujibu wa sheria
ili waendelee kuripoti wakati uchunguzi ukiendelea.
Uchunguzi bado unaendelea na baada ya
kukamailika yatakayobainika yatatolewa kwa mamlaka husika na kutelekezwa kwa
mujibu wa sheria kanuni na taratibu. Hivyo kila mmoja anatakiwa awe na subira
na uchunguzi unaofanywa na wataalam utakapokamilika mtajulishwa.
Ahsanteni kwa kunisikiliza
Imetolewa na:
David A. Misime -
SACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi.
No comments:
Post a Comment