Habari za Punde

Mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar Kati ya KVZ na Macho Manne Mchezo Uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Zanzibar.Timu ya KVZ Imeshinda bao 2-0

Kikosi cha Wachezaji wa Timu ya Machomane wanaoshiriki Ligi Kuu ya Zanzibar wakiomba dua kabla ya kuza kwa mchezo wao Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar na Timu ya KVZ.

Na Mwajuma Juma
MAAFANDE wa timu   ya Soka ya KVZ zimefanikiwa kutoka na ushindi katika michezo wao wa ligi kuu ya Zanzibar uliofanyika katika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.

Timu ya KVZ  imeshinda mchezo huo uliofanyika katika Mao Zedong na kufanikiwa kutoka na ushindi wa mabao 2-0, dhidi ya Timu ya Machomane.

Timu ya KVZ imeandika bao lake la kwanza katika dakika ya 56 lililofungwa na mshambuliaji wake Mabaadi Maulid Mabaadi na katika dakika ya 68 Madaadi Maulid Mabaadi akaandika bao la pili katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong .

Ushind wa JKU unaifanya kuendelea kuwa Katika nafasi yake ya tatu kwa kufikisha pointi 25 katika msimamo wa ligi hiyo inayoongozwa na KMKM wenye pointi 27, wakati KVZ kwa matokeo hayo KVZ wamefikisha point 18 na kupanda nafasi moja kutoka wa Saba hadi wa sita na kuwashusha Mafunzo ambao wana point  15.

Aidha katika uwanja wa Amaan timu ya Zimamoto ililazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Mlandege .

Zimamoto Katika mchezo huo ndio waliotangulia kupata bao dakika ya 10 tu kupitia kwa mchezaji wake Hamad Ibrahim Hilika alilolifunga kwa mkwaju wa penanti.

Mlandege kufungwa kwao huko hakukuawafanya wapote mwelekeo na badala yake walijirekebisha makosa yao na kufanikiwa kusawazisha ndani ya dakika ya 81 kupitia kwa Yahya Karoa.
Mshambuliaji wa Timu ya KVZ akiwapita mabeki wa Timu ya Machomane wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.Timu ya KVZ imeshinda mchezo huo kwa bao 2-0. 
Mchezaji wa Timu ya Macomane akijaribu kuzuiya mpira wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika katikac Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.Timu ya KVZ imesahinda mchezo huo bao 2-0.
Mshambuliaji wa Timu ya KVZ akimpita beki wa Timu ya Machomane wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar Timu ya KVZ imeshinda mchezo huo kwa bao 2-0.
Mshambuliaji wa Timu ya Machomane akijaribu kumpita beki wa Timu ya KVZ wakati wa mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.Timu ya KVZ imeshinda mchezo huo kwa bao 2-0.
Kocha Mkuu wa Timu ya KVZ King akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.
Kocha Mkuu wa Timu ya Machomane akitowa maelekezo kwa wachezaji wake wakati wa mapumziko katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Zanzibar uliofanyika Uwanja wa Mao Zedong Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.