Habari za Punde

Matukio Kutoka Bungeni Jijini Dodoma

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,  Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akizungumza na Mbunge wa Bariadi Mashariki, Andrew Chenge, bungeni jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji), Angellah Kairuki (kushoto) akizungumza na Waziri wa Nchi , Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu, bungeni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje, bungeni jijini Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Uwekezaji), Angellah Kairuki (kushoto) akizungumza na Waziri wa Madini, Doto Biteko, bungeni jijini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba , bungeni jijini Dodoma.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpongeza mwanamasumbwi, Salim Mtango wa Tanga ambaye Januari 31, 2020 alifanikiwa kumshinda kwa TKO bondia wa Thailand, Suriya Tarakhun na kunyakuwa mkanda wa dunia wa UBO. Bondia huyo alitembelea bunge jijini Dodoma Februari 6, 2020 kwa mwaliko wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu  (mwenye koti la bluu kulia). Wa tatu kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe na kushoto ni Naibu wake, Juliana Shonza. Kulia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Mendeleo Mijini, Angelina Mabula.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt, Harrison Mwakyembe kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mwita Waitara (kushoto) kwenye viwanja vya bunge jijini Dodoma, Februari 5, 2020. Wa pili kulia ni Mbunge wa Nachingwea, Hassan Masala na wa tatu kulia ni Mbunge wa Lindi, Hassan Kaunje. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.