Habari za Punde

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu Akutana na Wawekezaji wa Nishati ya Gesi


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu akiongea na wawekezaji wa Nishati ya kupikia aina ya gesi kutoka Kampuni ya KOPAGas. Kampuni hiyo imelenga kusambaza nishati ya gesi majumbani kwa gharama nafuu kwa mfumo wa ‘kulipia kadiri ya unavyotumia’ Wawekezaji hao wamemtembelea Waziri Zungu katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu akiongea na Bw. Stanslav Toldy raia wa Uingereza akiwa ni sehemu ya wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika uzalishaji wa magari yenye kutumia nishati ya umeme. Wawekezaji hao wamemtembelea Waziri Zungu katika Ofisi ndogo ya Makamu wa Rais, Mtaa wa Luthuli jijini Dar es Salaam. 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mussa Azzan Zungu hii leo ameungana na kikundi cha Pamoja Youth katika zoezi la Upandaji miti katika Shule ya Sekondari Buguruni-Moto. Takriban miti 100 imependwa katika eneo hilo ikiwemo miti ya matunda na miti ya vivuli.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.