Habari za Punde

JKU yatoa nyimbo maalum kutoa elimu juu ya maradhi ya Corona



Waimbaji wa kwaya wa kikundi Cha Utamaduni Cha Jeshi la Kujenga Uchumi JKU wakiimba wimbo wa Corona ugonjwa hatar uliotungwa na Mgazae Kinduli ambae pia ni mwamuzi msaidizi wa FIFA.

NA MWAJUMA JUMA
KIKUNDI Cha Utamaduni Cha Jeshi la Kujenga Uchumi JKU kimetoa nyimbo maalumu kwa ajili ya kutoa elimu juu ya maradhi ya Corona. 

Wimbo huo ambao utaimbwa kwa mtindo wa kwaya unatarajiwa kutoka muda wowote kuanzia leo na umetungwa na mtunzi wa nyimbo za kwaya wa Jeshi hilo,  Mgaza Kinduli na kuimbwa na wasanii Ramadhan Ameir, Hadia Waziri na Alhaj Madawa.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kinduli alisema kuwa unaitwa "Corona ni maradhi hatari",  lengo la kutoa wimbo huo ni kuhamasisha wananchi na jamii kwa ujumla juu ya kujikinga na kujilinda na maradhi hayo ambayo yameenea duniani kote.

Kinduli alisema kuwa tayari audio ya nyimbo hiyo imeshatoka na Sasa hivi wamo katika kuandaa vedio ambayo itatumika katika vituo vyote vya Zanzibar na Tanzania bara.

"Tayari audio imeshatayarishwa na muda wowote tutaisambaza huku tukiwa katika maandalizi ya mwisho ya kutoa video", alisema Kinduli.

Hii ni kwaya ya tatu  kwa mtunzi huyo kutoa ambayo ya kwanza ilihusu masuala ya Mapinduzi katika sherehe za kutimiza miaka 55 ya Mapinduzi na daftari la kudumu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.