Habari za Punde

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Balosi Seif Alim Iddi Aendelea na Ziara Yake Mkoani Shinyanga.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akiupongeza Uongozi wa Mgodi wa Mwadui wa Weilliamson Diamond Limited kwa jitihada zake za kuendeleza uzalishaji wa Madini ukihusisha Wafanyakazi wengi zaidi wanaouzunguuka Mgodi huo.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapi Mkoa wa Shinyanga Bibi Nyabaganga Dauth Taraba aliyesimama akitoa taafira fupi ya Wilaya yake wakati Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga Balozi Seif alipofika katikaMgodi wa Mwaduni kukagua uzalishaji wa Madini ya Almasi ndani ya Wilaya hiyo.
                                                        Picha na OMPR.
Na.Othman Khamis. OMPR.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema uamuzi wa Taifa la Tanzania kutaka kumiliki Rasilimali zake zote hasa zile za Madini umeonyesha muelekeo wa mafanikio katika Uimarikaji wa Uchumi wake ambao tayari umeanza kushuhudiwa na Dunia.
Alisema Mapato yanayotokana na Miradi ya Kiuchumi katika Sekta ya Madini pekee yameongezeka mara dufu kutokana na umiliki huo kwa sasa kuendeshwa kwa Ubia kati ya Serikali na Makampuni au Taasisi zilizofanikiwa kuingia Mkataba na Serikali Kuu kuendesha Miradi ya Madini hapa Nchini.
Balozi Seif Ali Iddi akiwa Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga alisema hayo wakati akiupongeza Uongozi pamoja na Wafanyakazi wa Mgodi ya Mwadui wa Williamson Diamond Limited  alipoutembelea unaozalisha Madini ya Almasi pekee Nchini Tanzania akiwa mwishoni mwa ziara yake ya Siku Tano Mkoani Shinyanga.
Alisema ongezeko la Uzalishaji wa Madini hayo ndani ya kipindi cha Awamu ya Tano ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli umewezesha kustawisha Maisha ya Wananchi wanaozunguuka Rasilmali hizo kwa kupata ajira inayokwenda sambamba na baadhi yao kushiriki kazi ya Uchimbaji wa Madini hayo.
Balozi Seif alisema Sekta ya Madini Nchini ilikuwa ikiendeshwa pamoja na kumilikiwa na Wageni kufuatia Sheria, sera na Mikakati iliyowekwa na Watawala wa Kikoloni na kutononesha  Mataifa na Familia zao kwa miaka mingi iliyopita jambo ambalo limeifanya Nchi kudorora Kiuchumi wakati imebarikiwa kuwa na Rasilmali za kutosha.
 “ Uamuzi wa Rais John Pombe Maguli wa kuirejesha Miradi ya Madini katika mikono ya Wananchi wenyewe umeanza kuleta faidfa na matumaini ya kutononoka kwa ustawi wa Wananchi wote”. Alisisitiza Balozi Seif .
Alifahamisha kwamba mfumo wa utaratibu uliowekwa hivi sasa katika mauzo yanayotokana na Madini Nchini uko wazi kiasi kwamba Wananchi kupitia Serikali Kuu wanaelewa kwa kina kiasi kinachozalishwa cha Madini, kile kinachopatikana baada ya uchekechuaji na thamani ya bei inayouzwa sokoni.
Akitoa Taarifa fupi ya Historia fupi ya Mgodi wa Mwadui wa Williamson Diamond Limited uliomo ndani ya Wilaya ya Kishapu Mkoani Mwanza Meneja Mkuu wa Mradi huo Mhandisi Ayoub Mwenda alisema Mgodi huo uliasisiwa mnamo Mwaka 1940 baada ya Mtaalamu wa Madini Raia wa Canada Bw. Williamson kugundua uwepo wa Madini ya Almasi eneo hilo.
Mhandisi Ayoub alisema mnamo Mwaka 1958 hadi Mwaka 1994 Mradi huo ulisimamiwa na Kampuni ya De Beers kwa kushirikiana na Shirika la Taifa la Madini  la iliyokuwa Serikali ya Kikoloni ya Tanganyika baada ya Mmiliki wa kwanza Bwana Williamson kufariki dunia.
Alisema Kampuni hiyo iliamua nafasi yake kuiuza kwa Kampuni nyengine ya Petra hadi Mwaka 2010/2011 pale Serikali Kuu iliposimamisha uzalishaji kutokana na mapato madogo yaliyotokana na uchakavu wa Mitambo yake.
Meneja Mkuu huyo wa Mgodi wa Mwadui alimueleza Mlezi wa Mkoa wa Shinyanga kwamba utafiti uliofanywa na Wataalamu wa Mgodi huo umebaini kwamba Shimo la Mchanga lenye ukubwa wa Hekta 146 likiwa na Mita 580 kutoka usawa wa Ardhi limebainisha Uwepo wa utajiri mkubwa wa Mchanga unaofikia Tani Bilioni Moja.
Alisema Utafiti huo ulikwenda samba na mpango wa muda mrefu unaoendesha mradi huo hadi Mwaka 2038 licha ya kwamba Mgodi huo kuwa na uwezo wa kufanya kazi katika kipindi cha zaidi ya Miaka 100 kutoka hivi sasa baada ya Utafiti na Mpango huo.
Mhandisi Ayoub alifafanua kwamba Mpango na Utafiti huo utawasaidia Watendaji na Wataalamu wa Mgodi huo wapatao 532 kubaini mahitaji halisi ya Mashine zitakazokuwa na uwezo wa kufanyakazi kulingana na Miamba ilioyopo hadi kipindi hicho cha Mwaka 2038.
Naye Afisa Uhusiano wa Mgodi wa Mwadui Nd. Joseph Kazi alisema alisema upo Mpango wa Maendeleo ya Jamii wa Mgodi huo tokea uzalishaji wake ulipohusishwa na Jamii inayouzunguuka Mradi huo muhimu kwa Maendeleo na Ustawi wa Wananchi waliowengi.
Nd. Kazi alisema zaidi ya Vijiji Kumi na Moja vilivyouzunguuka Mgodi wa Mwadui vimeanza kufaidika na huduma za Afya, Maji, Elimu kwa kuondosha changamoto ya Vikalio ndani ya Shule zote za Wilaya ya Kishapu kwa kukabidhi Madawati Elfu 4,919, huduma za Akina Mamapamoja na Vijana.
Alisema shughuli hizo zinakwenda sambamba na uoteshaji wa Miti katika maeneo ya machimbo ili kurejesha uasili uliyopo awali baada ya kuanzisha Kitalu cha miti ndani ya Mgozi huo.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bibi Nyabaganga Dauth Taraba alisema yapo mabadiliko makubwa ya Kiuchumi yaliyopatikana kwa Wananchi wa Wilaya ya Kishapu kupitia Mradi wa Almasi uliopo Mwadui kuanzia Mwaka 2015 hadi hivi sasa.
Bibi Nyabaganga alisema kufunguliwa kwa mnada wa mauzo ya Madini ya Almasi kuanzia Mwaka huu  ambapo asilimia 5% ya kinachozalishwa kuwarejea Wananchi ni tukio la Historia kwa Tanzania ambalo halijawahi kutokea tangu kuanza kwa uzalishaji wa Sekta ya Madini Nchini Miaka 70 iliyopita.
Alisema uwepo wa Mradi huo unaokwenda sambamba na jitihada za Serikali  Kuu katika kusogeza huduma muhimu kwa Jamii imepelekea kupungua kwa vifo vya Mama na Watoto kutokana na kuongezeka kwa Hospitali na Vituo vya Afya, kuimarika kwa zao la Pamba pamoja na ongezeko la Ufaulu wa Wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.