Habari za Punde

Viongozi Watakiwa Kufuata Maadili ya Uongozi

Na.Takdir.Suweid. 
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Magharibi Ndg.Mohammed Rajab Soud amewataka Viongozi wa Majimbo kuendelea kutekeleza Ilani ya chama hicho na kuacha kuwagawa makundi Wananchi wao.

Amesema baadhi ya Viongozi hawatekelezi majukumu yao na badala yake wanapita mitaani kupiga kampeni na kuwachafua wenzao.

Akizungumza katika Mkutano wa kueleza utekelezaji wa ilani ya CCM kwa Viongozi wa Jimbo la Pangawe huko Kiwanja cha Mpira Nyarugusu amesema Viongozi hao kupita mitaani kwa kupiga kampeni muda huu ni kinyume na Maadili ya Uongozi na atakaebainika jina lake halitorudishwa wakati atakapoomba ridhaa kwa mara nyengine.

Amewaomba Wananchi watakaowabaini Viongozi kuenda kinyume kupeleka Taarifa sehemu husika ili wachukuliwe hatua za kinidhamu.

Mbali na hayo amewakumbusha Viongozi hao kuendelea kuwatumikia Wananchi na kuacha kupiga Kampeni ili kujikinga na athari zinazoweza kujitokeza.

Hata hivyo amewakumbusha Wananchi kuchaguwa Viongozi wenye uchungu wa nchi ambao watawaletea maendelo katika maeneo yao na kuacha ubabaishaji.

Nao Viongozi wa Jimbo la Pangawe wamesema tayari wameshatekeleza Ilani kwa asilimia kubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo ya Maji,Umeme,Afya,Njia za ndani,Vikundi vya Vijana na Wanawake na kuwaomba Wananchi kuwaunga Mkono ili wazidi kuwatumikia.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.