Habari za Punde

Dkt Mwakyembe atoa salamu za pole kwa mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania


  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO                                          
                                  SALAMU ZA POLE

                                           
TAARIFA KWA UMMA
Aprili 1, 2020 Dodoma.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (Mb) ametoa pole kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Habari Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba kwa kuondokewa na Mwanahabari Nguli Bw. Marin Hassan Marin leo asubuhi Jijini Dar es Salaam.

Akiongea moja kwa moja na televisheni ya TBC 1, Dkt. Mwakyembe ameeleza kuwa TBC na tasnia ya habari kwa ujumla imepata pigo kwani Bw. Marin alikuwa mstari wa mbele kuhakikisha sekta ya Habari inakuwa  na mchango chanya katika maendeleo ya jamii.

 Enzi za uhai wake marehemu alikuwa mmoja wa waasisi wa vipindi kadhaa vya TBC vikiwemo Jambo Tanzania, Nyumba ya Jirani na Aridhio.  

Dkt. Mwakyembe ametoa pole kwa familia, ndugu,jamaa,marafiki na wadau wote wa tasnia ya habari nchini.

Imetolewa na

Lorietha Laurence
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.