Habari za Punde

Mawaziri wa Habari wa SMT na SMZ Waongozi Wananchi Katika Maziko ya Mwandishi Mwandamizi Mtangazaji wa TBC Marehemu Marin Hassan Marin Yaliofanyika Leo Jijini Zanzibar na Kuzikwa Makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi "B" Unguja Waziri Mwakyembe

Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar. Mhe. Mahmoud Thabit Kombo na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakihudhuria maziko ya Mwandishi Mwandamizi  wa Shirika la Habari Tanzania (TBC ) Marin Hassan Marin, wakielekea katika Msikti wa Kibweni KMKM kwa ajili ya kumuombea Dua na Sala  na kuzikwa katika Makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi "B" Unguja leo asubuhi saa nne.
Waumini wa Dini ya Kiislam wakishiriki katika Sala ya kuuombea Mwili wa Marehemu Marin Hassan Marin, iliyoongozwa na Sheikh Mohammed Iddi Thabit ilioyofanyika katika Msikiti wa Kibweni KMKM, na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi "B" Unguja leo.
Waumini wa Dini ya Kiislam Zanzibar wakiitikia Dua baada ya kumaliza Sala ya kuusalia mwili wa Marehemu Marin Hassan Marin, Mwandishi Muandamizi Tanzania wa TBC, iliofanyika katika Msikiti wa Kibweni KMKM leo na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi"B" Unguja  
Wananchi wakiwa wamebeba jeneza lililokuwa na Mwili wa Marehemu Marin Hassan Marin wakitoka katika Msikiti wa Kibweni KMKM baada ya kumalizika kwa Sala na Dua ya kumuombea na kuzikwa katika makaburi ya Mwanakwerekwe Wilaya ya Magharibi "B" Unguja leo.


Wananchi na Wafanyakazi wa vyombo vya habari Tanzania Wakijumuikka na Mawaziri wa Habari wa SMT na SMZ katika makaburi ya Mwanakwerekwe wakishiriuki katika maziko ya Mwandishi wa Habari na Mtangazajiu wa TBC Marehemu Marin Hassan Marin yaliofanyika leo katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar.
Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislam wakiitikia Dua ya kumuombea Marehemu Marin Hassan Marin baada ya kumalizika kwa maziko yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar. 
Wananchi na Waumini wa Dini ya Kiislam wakiitikia Dua ya kumuombea Marehemu Marin Hassan Marin baada ya kumalizika kwa maziko yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar. 
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Ayoub Rioba akizungumza na kutowa Wasifuu wa marehemu Marin Hassan Marin, wakati wa hafla ya maziko hayo yaliofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Jijini Zanzibar Wilaya ya Mjini Magharibi "B" Unguja yaliofanyika leo. 
Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombo akizungumza na kutowa salamu za SMZ na kutoka shukrani kwa TBC, wakati wa hafla ya maziko ya Mwandishi wa Habari na Mtangazaji Muandamizi Tanzania Marehemu Marin Hassan Marin yaliofanyika katika makaburi ya mwanakwerekwe Jijini Zanzibar Wilaya ya Magharibi "B" Unguja leo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na kutowa poile kwa Familia ya Marehemu na kuwasilisha Salamu za Wizara yake wakati wa hafla ya maziko ya Mwadishi wa Habari na Mtangazaji wa TBC Marehemu Marin Hassan Marin yaliofanyika leo katika makaburi ya mwanakwerekwe Jijini Zanzibar Wilaya ya Magharibi "B" Unguja. 
Mwakilishi wa Familia akizungumza na kutoka shukrani kwa Serikali za SMZ na SMT kwa msaada wao mkubwa katika  kufanikisha maziko ya Kijana wao.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.