Habari za Punde

MKUU WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI AFANYA MABADIKO YA MAKAMNDA


                    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
                   WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
                               JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
OFISI YA KAMISHNA JENERALI
    JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI
          S. L. P. 1509,
             DODOMA.
          02 APRILI, 2020
 
  
Simu ya maandishi: “ZIMAMOTO KUU”
Simu Nambari:  +255-22-2113537
Telefax:           +255-22-2184569
Dharura simu Nambari 114
                

         TAARIFA KWA UMMA
Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF) John W. Masunga, amefanya mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Mikoa.

Makamanda walioguswa na mabadiliko hayo ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Zimamoto na Uokoaji (SACF) ABDALLAH MAUNDU anakwenda kuwa (RFO) Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kigoma, kabla ya nafasi hii alikuwa Makao Makuu Dodoma.

Aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) SALUM M. OMARI, anayekwenda kuwa (RFO) Kamanda wa Mkoa wa Kinondoni, kuchukua nafasi ya Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji (ASF) JENIFER V. SHIRIMA anayehamia Makao Makuu kuwa Mkuu wa dawati la Mambo ya Nje.

Aidha nafasi ya (RFO) Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara inachukuliwa na Mrakibu Msaidizi wa Zimamoto na Uokoaji (ASF) AUGUSTINE B. MAGERE.

Pia aliyekuwa Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) ELIA P. KAKWEMBE, anayekwenda kuwa (CFO) Kamanda wa Viwanja vya Ndege Nchini, kuchukua nafasi ya Kamishna Msaidizi (ACF) BAKARI K. MRISHO anayekwenda kuwa (RFO) Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Temeke.

Aliyekuwa Kamanda wa  Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga Mrakibu wa Zimamoto na Uokoaji (SF) OMARI H. SIMBA anayekwenda kuwa (RFO) Kamanda wa Mkoa wa Simiyu na nafasi yake inachukuliwa na Mrakibu wa  Zimamoto na Uokoaji (SF) GEORGE G. MRUTU anayetoka Makao Makuu.

Mabadiliko haya ni ya kawaida kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

KUOKOA MAISHA NA MALI NI JUKUMU LETU SOTE


Imetolewa na;       

Joseph Mwasabeja – (INSP)
Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji
Makao Makuu
S. L. P 1509

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.