Habari za Punde

Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Wilaya ya Kati Unguja Mhe. Mohammed Raza Akabidhi Msaada wa Vitu Mbalimbali Kwa Ajili ya Kupambana na Corona Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed akisalimiana na  Mwakilishi wa Jimbo la Uzini na Mfanya Biashara maarufu Mohamed Raza kwa njia ya kugongana Miguu katika hafla ya upokeaji Msaada wa Vitu mbalimbali vilivyotolewa na Mwakilishi huyo kwa ajili ya kupambana na Maradhi ya Korona  iliofanyika nje ya ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil Kikwajuni Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed (kulia)akizungumza baada ya kupokea Msada wa Vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mchele ,Magodoro, Mashuka Taula, Dawa za kuosha mikono Vilivyotolewa na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini na Mfanya Biashara maarufu Mohamed Raza kwa ajili ya kupambana na Maradhi ya Korona hafla iliofanyika nje ya ukumbi wa Sheikh Idriss Abdul wakil Kikwajuni Zanzibar.

Picha na Yussuf Simai - Maelezo  Zanzibar.No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.