Habari za Punde

Umoja wa Mataifa Waonya Juu ya Baa la Njaa la 'Kibiblia'

 
Dunia iko katika hatari ya kusambaa kwa njaa "sawa na za zama za kale za Kibiblia" kutokana na janga la virusi vya corona, umeonya Umoja wa Mataifa.
Mkuu wa shirika ka mpango wa chakula duniani (WFP), David Beasley, amesema kuwa hatua ya dharura inahitajika ili kuepuka maafa .
Ripoti imekadiria kwamba idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa inaweza kupanda kutoka watu milioni 135 hadi zaidi ya watu milioni 250.
Walio katika hatari zaidi ni wanaoishi katika nchi 10 zilizoathiriwa zaidi na mizozo ya kivita, mzozo wa kiuchumi na mabadiliko ya hali ya hewa, limesema shirika la WFP.
Ripoti ya nne ya mwaka juu ya mzozo wa dunia wa chakula, imezitaja nchi za Yemen Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo Afghanistan, Venezuela, Ethiopia, Sudan Kusini, Sudan, Syria, Nigeria na Haiti kuwa ndizo zitakazoathiriwa zaidi.
Nchini Sudan Kusini, 61% ya watu waliathiriwa na mzozo wa chakula mwaka jana, inasema ripoti hiyo.
Hata kabla ya janga la virusi vya corona, baadhi ya maeneo ya Afrika Mashariki na Asia Kusini yalikua tayari yanakabiliwa na upungufu mkubwa chakula uliosababishwa na ukame pamoja na uwepo wa nzige ambao haujawahi kushuhudia kwa miongo kadhaa.
Alionya wazi kuwa : "Kwa namna moja au nyingine, dunia itagarimia kwa hili."Bora kufanya kazi pamoja, alisema, kwa misingi ya kweli ,sio hofu."
Mchumi wa ngazi ya juu wa WFP, Arif Husain, amesema kuwa athari ya kiuchumi ya janga la corona inaweza kusababisha maafa kwa mamilioni ya watu "ambao tayari wanakabiliwa na njaa".
"Ni sawa na kupigwa kwa nyundo kwa mamilioni zaidi ya watu ambao wanaweza kula tu iwapo watapata malipo ," alisema katika taarifa.
"Sheria za kukaa nyumbani na kudorora kwa uchumi tayari vimewaathiri. Wanapopatwa na mshituko mmoja tu-kama wa Covid-19 - unawaathiri sana. Lazima tuchukue hatua kwa pamoja sasa hivi kuzuwia athari za janga hili la dunia "
Mapema mwezi huu, WFP lilisema linapanga kupunguza msada katika baadhi ya maeneo yaliyokumbwa na vita nchini Yemen yanayodhibitiwa na waasi wa Houthi kutokana na ukosefu wa fedha za udhamini.
Lilisema baadhi ya wahisani wamesitisha msaada wao kutokana na hofu kwamba misaada yao inazuwiwa vikosi vya Kihudhi.
Shirika la WFP huwalisha Wayemen zaidi ya milioni 12 kwa mwezi, 80% miongoni mwao wakiishi katika maeneo yanayodhibitiwa na Vikosi vya Kihuthi.
Yemen ilithibitisha kisa chake cha kwanza cha Covid-19 mapema mwezi huu, huku mashirika ya misaada yakionya kwamba ugonjwa huo unaweza kufikia haraka kiwango cha kutoweza kushughulikiwa na mifumo ya taifa hilo ya afya iliyodhoofika
Chanzo cha Habari.BBC.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.