PRESS
RELEASE
MAKABIDHIANO YA
MISAADA KUTOKA UMOJA WA
WAZALENDO NA
WAFANYABIASHARA KATIKA
MAPAMBANO DHIDI YA
VIRUSI VYA KORONA
3 APRIL
2020
On
Behalf of the entire Business Community, Patriotism and Friends of Zanzibar
both in Mainland Tanzania and Zanzibar
Telephone: 0779 060 338
PRESS
RELEASE
Mheshimiwa
Waziri
Kwanza nitoe shukrani kwa niaba ya
Umoja wa Wazalendo na wafanyabiashara kwako Mhe. Waziri, kwa kuchukua muda wako
kujumuika nasi katika shughuli yetu ya leo ya makabidhiano ya bidhaa , madawa
na vifaa vilivyoochangwa au kutolewa na wafanyabishara, Wazalendo na Marafiki
wa Zanzibar
Natambua majukumu makubwa ulionayo ya
kitaifa, lakini umeweza kulipa uzito suala hili. Tunakushukuru sana!
Vile vile ninawashukuru
wafanyabiashara, Wazalendo, Marafiki wa Zanzibar, Taasisi na watumishi wa umma
waliojitokeza na kutuunga mkono katika juhudi zetu za kupambana na mlipuko huu wa
virusi vya korona (Covid19 outbreak).
Mheshimiwa
Waziri
Ni miezi mitatu imepita tangu ugonjwa hatari wa korona umeingia duniani.
Kasi ya kusambaa kwa ugonjwa huu inazidi kuongezeka na hatimaye ugonjwa huu
umefika nchi nyingi za Afrika ikiwemo Tanzania. Katika kuunga mkono juhudi za
Mhe Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein na Serikali
yake, Umoja huu wa Wafanyabiashara na Wazalendo Tanzania Bara na Visiwani haukubaki
nyuma katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu, tangu uliporipotiwa duniani na
hata ulipotangazwa kuingia hapa nchini. Tunatambua kuwa, tayari serikali
imeweka mikakati mahususi ya kupambana na ugonjwa huu na kuhakikisha
wafanyabiashara na wananchi wamejiandaa na athari zinazoweza kusababishwa na
ugonjwa huu wa Covid19 kiuchumi, kiafya na kijamii kwa ujumla.
Mheshimiwa
Waziri
Kwa kutambua na kuunga mkono juhudi
za Mhe Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar Dr Ali Mohammed Shein na Serikali yake kwenye afya, naomba niwasilishe
Architectural Drawings (Ramani ya mchoro) wa Laboratory Level 3 ambayo
kungepenga kuwasilisha kwa serikali na kama ikiwapendeza serikali, tuje tukae
chini kuangalia namna ya kuisadia Serikali kiujenzi na kwa vifaa
Mheshimiwa
Waziri
Umoja huu; umeleta mshikamano wa pamoja
wa wafanyabiashara na taasisi mbalimbali za kibishara na umekuwa ukitoa ushirikiano
wa karibu kwa Serikali (Public Private
Partnership – PPP) katika kuhakikisha kuwa mapambano dhidi ya ugonjwa huu
yanaleta ushindi.
Mheshimiwa
Waziri
Ushirikiano na moyo wa uzalendo
uliopo kati ya umoja huu wa Wazalendo na Wafanyabiashara nchini umewezesha
kuunganisha nguvu na hatimaye kufanikisha kupatikana kwa vifaa mbalimbali
vyenye thamani ya shilingi 126 milioni vitakavyosaidia kwenye mapambano dhidi ya
ugonjwa wa corona.
Naomba nitoe orodha ya wale wote waliochangia
Explain
the HOTSPOTS areas identified: Malindi
Port;Stone Town; Marikiti; Kivingo Beach; Mnazi Mmoja Hospital; Kiinua Miguu
Prison; Soko La Mwanakwerekwe; Bububu; Forodhani Park; Kituo cha Mabasi
Airport; Darajani; Soko la Saateni; Mlandege; Michenzani; Kariakoo; Rahaleo; Mwembeladu
Hospital; Jangombe; Mombasa; Mwera; Ngungwi Beach; Kiwengwa; etc.
Mheshimiwa
Waziri
Umoja wa Wazalendo na ya
wafanyabiashara nchini, wakubwa kwa wadogo wote tumeguswa na tumewiwa kutoa
ushirikiano kwa Serikali, jamii na kwenye maeneo yetu ya kazi kuhakikisha kuwa
tunapambana kikamilifu na ugonjwa hatari wa corona. Napenda tukuhakikishie Mhe Waziri kuwa Umoja huu
wa Wazalendo na Wafanyabiashara nchini utaendelea kushirikiana na serikali na
wadau wengine hadi pale ambapo ugonjwa huu utakapodhibitiwa kikamilifu.
Mheshimiwa
Waziri
Ushiriki wa Umoja huu katika
mapambano dhidi ya ugonjwa wa corona haukwepeki!!. Pamoja na nia njema ya umoja
huu, ikumbukwe pia kuwa umoja huu ambao ndio nguzo ya sekta binafsi una mchango
mkubwa katika kujenga uchumi wa nchi na ndiyo sekta inayozalisha ajira nyingi
nchini kwa takribani asilimia 80. Mheshimiwa
Waziri, Sekta Binafsi tunashiriki kwa asilimia mia moja katika mapambano
dhidi ya corona kwa kuwa sisi ni sehemu ya jamii. Tusipofanya hivyo, hakuna
atakayebaki salama; na hata biashara zetu zitakufa pia. Mheshimiwa Waziri, kila jambo linahitaji watu. Nchi inahitaji watu.
Maendeleo yanahitaji watu. Biashara pia zinahitaji watu, hivyo tuna kila sababu
ya kushiriki kujilinda na kuwalinda wengine,”
Mheshimiwa
Waziri
Vile vile Umoja huu unaipongeza
Serikali kwa hatua na juhudi makini ilizochukua hadi sasa. Hatua hizo ni pamoja
na kuwahamasisha watanzania kuchukua tahadhari na kuwa makini wakati wote kwani
Kila mtu akitekeleza wajibu wake wa kujilinda yeye binafsi na kuwalinda wengine
tutaweza kuvuka kwa mafanikio makubwa, hasa ikizingatiwa kuwa walio wengi
wanapona hata baada ya kupata maambukizi ya ugonjwa huu
Mheshimiwa
Waziri
Kabla ya kumaliza hotuba yangu naomba
nitoe shukrani kubwa sana kwako, kwa walio hapa na wasiojaaliwa kuwepo ambao
wameshiriki kwa hali na mali nikianzia na:
Mzee wangu Subhash Patel; Motisun and
CTI Chairman
Mr Mohammed Bhaloo, Chairman Agha
Khan Trust for Culture Zanzibar
Said Salim Bakhresa (Bakhresa Group)
Dhruv Jog, Advent Construction
Dr. Mohammed Ali, SADC Medical Expert
Abubakar Said Salim Bakhresa
Ambassador Antonio, Brazil (Personal Contribution)
Dr Maryam Lymo, Innovative Projects
Balozi Kindamba
Hamad
Hamad, Zanzibar Chamber of Commerce
Mr. Rahim Bhaloo, Multi Color Printers Ltd
Parvin
Hasnein
Asha
Aslan
Lukman
Fideli Ali
Farid
Fazach
Aboud
Nassor Khamis
Nafisa
Jidawi, Wajamama
Zanzibar
Sugar Factory Ltd
Skylink
Travel & Tours
AZAM
Marine Co Ltd
Amsons
Group
Camel
Oil
Association
of Tanzania Oil & Gas (ATOGS)
ORYX
Energies
Tridea
Cosmetics Ltd
Majid Store
Aruna Pharmacy
Patel Import & Export
Bharat
Enterprises
Kay
Sotta
Plastic
Limited
Print
Plus
Mozeti
Virgo Group
Print Plus
Ashton Media
Pamoja na wote waliotoa michango yao
ya hali na mali .
Umoja ni nguvu, Utengano ni Udhaifu
Mshikamano Daima!
Asanteni
sana
No comments:
Post a Comment