Habari za Punde

Wananchi wa Jimbo la Pangawe Watakiwa Kuanzisha Kamati Kusaidia Kuondoa Kero.

Na.Takdir Suweid -Maelezo Zanzibar.
Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe Mhe. Khamis Juma Mwalim amewataka Wananchi wa Jimbo hilo kuanzisha kamati zitakazosaidia kutatua matatizo madogo madogo yanayowakabili na kuacha kutegemea Viongozi pekee.
Ameyasema hayo wakati alipokuwa katika ziara ya kukagua Ujenzi wa Kisima cha Maji huko Mnarani Wilaya ya Magharibi “B” Unguja.
Amesema Viongozi wanamajukumu  mengi ya kuwatumikia Wananchi wao hivyo muda mwengine wanashindwa kutatua matatizo yote yanayowakabili katika maeneo yao.
Aidha amesema Kamati hizo zitasaidia kujadili mbinu za kuzipatia Ufumbuzi Kero zilizopo ikiwepo kuharibika mashine ya kusukumia maji na michango ya umeme wa kuendesha Kisima hicho.
Hata hivyo amewapongeza Wananchi hao kwa Uzalendo waliouonyesha wa kutoa eneo na kunzisha michango ya ujenzi wa kisima hicho jambo ambalo limesaidia kupata ufadhili ufadhili wa haraka.
Nae Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo Jimbo la Pangawe Zanzibar Ndg. Ali Jaku amewataka kuacha kuingiza masuala ya ubaguzi wa kisiasa katika kamati hiyo sambamba na kujumuisha Wanawake ili watowe michango yao kwani ndio waathirika wakubwa wa tatizo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.