Habari za Punde

Kupingwa kwa amri ya kukaa ndani inayoendelea nchini Marekani

Katika nyakati hizi, kuona mkutano wa hadhara wa mamia ya watu wengi bila bila barakoa ni jambo linalotisha.
Lakini hiyo ndio ilifanyika katika maandamano dhidi ya hatua za kusitisha shughuli mbalimbali katika jimbo la Washington.
"Tunaamini kuwa gavana wa jimbo hilo amekwenda zaidi ya mamlaka yake ya kikatiba katika kufunga biashara na kuagiza watu kukaa nyumbani," mratibu Tyler Miller ameeleza.
Katikati mwezi ya Machi, Gavana wa Washington Jay Inslee alitangaza hali ya dharura kama ilivyofanyika katika maeneo mengi ulimwenguni; kufunga migahawa vilabu vya pombe na kupiga marufuku mikusanyiko mikubwa.
Lakini waandamanaji wanasema katiba ilikiuka.
"Katiba ya serikali ya jimbo inasema kwamba haki ya watu ya kukusanyika kwa amani haitabadilishwa kamwe. Tunaamini kwamba matamshi ya (dharura ya virusi vya corona) ambayo gavana aliamuru, ilikiuka hayo," Bwana Miller anasema.
Bwana Miller alisema hakuwa akipinga maagizo kutoka kwa mashirika ya afya ya Umma na anaheshimu hilo
"Hata nilijiweka karantini siku 14 , tangu awali, wakati nilipokuwa na ugonjwa ambao ulionyesha dalili kadhaa," anasema.
"Ukweli mimi ninaandamana haimaanishi nadhani ni wazo nzuri kuwa na mikusanyiko, ninaamini tu kwamba serikali haina mamlaka ya kuwazuia."
Katika wakati wote wa shida, Bwana Miller ameweza kuendelea na kazi yake kama fundi wa uhandisi katika Jeshi la wana maji nchini Marekani.
Vizuizi hutofautiana kutoka jimbo hadi jimbo, na takriban majimbo 20 yamekuwa na maandamano dhidi ya hatua hizo. Maonesho haya yanatofautiana katika ukubwa kutoka kwa watu kadhaa hadi , maelfu.
Bado viwango vya vifo nchini Marekani kutokana na Covid-19 havijashuka na bado kelele za kuondoa vikwazo haziko tu kutoka kwa wananchi wa kawaida, lakini kutoka kwa wanasiasa pia.
"Kulikuwa na hatua za serikali za haraka kuhusu suala la lazima la kufunga shughuli mbalimbali,'' anasema.
maelfu ya watu wamekufa kote nchini Marekani na kwamba idadi ingeweza kubwa zaidi kama kusingekuwa na marufuku zaidi.
"Hilo ni jambo ambalo utaweza kusema bila kujali; kwamba kunaweza kuwa na vifo zaidi," anasema Bw Becker, ambaye pia ni daktari aliyehitimu.
"Unachukua hoja ya 'ikiwa itaokoa maisha ya mtu mmoja', na ningesema kwamba ikiwa ningeendesha gari kwa kasi ya 20mph badala ya 50mph, inawezekana kwamba siwezi kumuua mtu, na unaweza kuangalia nyanja zote za maisha yetu. Lakini njia yetu yote ya maisha katika nchi hii itaanguka na hatuwezi kuishi maisha kama hayo. "
Katika jimbo la jirani Dakota Kusini, mmoja wa wale waliokufa na ugonjwa huo alikuwa Bob Glanzer, mwakilishi wa serikali.
"Alikuwa mtu anayejali sana, mwenye kujitoa, kusikiliza, na hakika imani ilikuwa sehemu kubwa ya maisha yake. Atakumbukwa sana katika bunge," anasema mwenzake wa chama hicho Jean Hunhoff.
"Kwa kweli kwa Donald Trump sio siri kuhusu anachofikiria, yeye husema tu. Nadhani kuna ushahidi mwingi kwamba ana wasiwasi kuwa ugonjwa huu mbaya na namna unavyoshughulikiwa katika hatua za mwanzo, pamoja na athari za kiuchumi, kuzama kwa urais wake, "anasema.
"Hauwezi kutarajia yeye, chama chake na wale wanaomuunga mkono kukaa na kuchukulia juujuu suala hili , kwa hivyo mpango B au C ni nini? Ni kutoka kwa kumlaumu Obama, Wachina, WHO, hadi sasa kuwalaumu wale ambao wanaweka marufuku mbalimbali "
Hakika, kwa wiki za hivi karibuni, Donald Trump amewaunga mkono waziwazi waandamanaji.
Lakini ujumbe mchanganyiko kutoka Ikulu ya Marekani imekuwa sehemu ya shida hii. Baada ya kuashiria kwamba alitaka majimbo mengine yanayoongozwa na Democratic kidemokrasia "yapewe uhuru" na kufunguliwa, rais kisha akasema alikuwa "hana furaha" wakati gavana wa Republican wa Georgia alifanya uamuzi wa kuufungua tena uchumi.
Pamoja na mami kufa kwa virusi kila siku, watawala wa serikali za majimbo wapo katika nafasi ngumu ya kujaribu kufanya maamuzi sahihi ya kuwaweka salama watu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.