Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza na Wajumbe wa Kamati
ya Taifa ya Huduma kwa Jamii kabla ya kuzindua Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo,
ambayo itasimamia Utekelezaji wa Sheria ya Huduma kwa Jamii inayotoa fursa kwa
wafungwa wa vifungo vidogo kutumikia adhabu hizo kwenye jamii. Pia Waziri huyo
ameitaka Kamati hiyo, iweke mikakati zaidi ya kusimamia adhabu mbadala ya
kifungo cha nje ili kuondoa msongamano magerezani.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati meza kuu),
akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, alipokuwa
akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii kabla uzinduzi wa
Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia), akimsikiliza Katibu wa
Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Huduma za
Uangalizi, Aloyce Musika, alipokuwa anazungumza kabla ya kabla uzinduzi wa
Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo. Waziri Simbachawene amezindua Kamati hiyo,
ambayo itasimamia Utekelezaji wa Sheria ya Huduma kwa Jamii na kutoa fursa kwa wafungwa
wa vifungo vidogo kutumikia adhabu hizo kwenye jamii. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Jaji Zephrine Galeba.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (katikati meza kuu), akimsikiliza
Mjumbe wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa Jamii, Isaac Nantanga (kushoto), wakati
alipokuwa anajitambulisha kabla ya uzinduzi wa Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo.
Watatu kulia ni Katibu Mkuu, Christopher Kadio.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (wanne kushoto), Katibu Mkuu,
Christopher Kadio (wanne kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Huduma kwa
Jamii, Jaji Zephrine Galeba (watatu kushoto), Katibu wa Kamati, Aloyce Musika
(watatu kulia), Kamishna Jenerali wa Magereza, Suleiman Mzee (wapili kulia),
wakiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Kamati hiyo, jijini Dodoma, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment