Habari za Punde

Serikali Yasisitiza Kutoa Ushirikiano kwa Wasanii

  Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimpongeza Msanii wa Filamu Bw. Ezekiel Mwakipageme maarufu kama Soudblack (wa kwanza kushoto) anayefanya kazi za filamu nchini China kwa mpango wake wa kushirikiana na wasanii wenzake watanzania katika kukuza tasnia ya filamu nchini wakati msanii huyo alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dodoma.
 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akimsikiliza Msanii wa Filamu Bw. Ezekiel Mwakipageme maarufu kama Soudblack (wa (kwanza kushoto) kuhusu mpango wake kuendeleza tasnia ya filamu nchini wakati msanii huyo alipomtembelea ofisini kwake leo Jijini Dodoma.
 Mtayarishaji na Mwongozaji wa Filamu Tanzania Bw. John Kalaghe (wa kwanza kushoto) akifafanua jambo kwa Mhe. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) kuhusu kazi za filamu wanazotarajia kuzifanya kwa kushirikiana na Msanii Bw.Ezekiel Mwakipageme maarufu kama Soudblack (wapili kushoto) ofisini kwa Mhe.Waziri leo Jijini Dodoma.

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Msanii wa Filamu nchini China, Bw.Ezekiel Mwakipageme maarufu kama Soudblack (wa pili kushoto) mara baada ya kufanya nae mazungumzo ofisini kwake leo Jijini Dodoma.

Na.Adeladius Makwega -WHUSM
Serikali imesisitiza kuendelea kutoa ushirikiano kwa wasanii kupitia vyombo na idara zake zinazosimamia sekta hiyo ili kusaidia kazi zao kufahamika zaidi ndani na nje ya nchi.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe wakati alipotembelewa na msanii Ezekiel Mwakipageme maarufu kama Sud Black ambaye ni msanii wa sanaa ya maigizo.

Waziri Mwakyembe amesema kuwa sanaa ya Tanzania inapofanyika sehemu yoyote ni vizuri kuwa ya mfano na yenye motisha kwa wale wanaotaka kufanya kazi za sanaa pamoja na wale wanaozifuatilia kazi hizo.

“Hongera kwa kucheza picha nyingi, kuigiza na wasanii wengi wakubwa na kwa kufanya hivyo umeweza kuibeba na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania huko nchini China na kimataifa.” Amesema Waziri Mwakyembe.

Kwa upande wake, msanii Ezekiel Mwakipageme amesema kuwa anatarajia kuwakaribisha wawekezaji kutoka China kuja kuwekeza katika ulimwengu wa filamu kwa kujenga studio ya kisasa, chuo cha michezo na pia kufungua miradi mingine ya maendeleo ikiwemo huduma za afya.

“Nimecheza filamu nyingi na wasanii wakubwa kama Jack Chain na wengine na hivi karibuni zitatoka filamu zangu mpya mbili, Watanzania watarajie mengi makubwa katika tasnia hii ya filamu”, Alisema msanii Sud Black.

Nae Mtayarishaji wa Filamu, John Kalage ambaye ndiye Mkurugenzi wa msanii huyo hapa nchini Tanzania ameishukuru Serikali kwa ushirikiano wanaoutoa katika masuala yote ya Filamu na Sanaa. kufanya kazi zetu kwa kufuata miongozo yote ya serikali na kuondoa migongano isiyo ya lazima”, Amesema Mkurugenzi Kalage.

Serikali ya Awamu ya Tano kama ilivyotoa ahadi yake ya kukuza sanaa na wasanii kwa kufanya kazi za sanaa kuwa ajira kwa vijana imeendelea kutekeleza ipasavyo huku baadhi ya wasanii wakiendelea kuibuka na kazi zao kuvuka mipaka ya taifa letu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.