Habari za Punde

Waziri mkuu wa Uingereza kutoa maelezo ya kuondoa marufuku ya kukaa nyumbani

Waziri Mkuu wa Ungereza Boris Johnson anatarajiwa kutoa maelezo zaidi wa kurejesha hali ya kawada nchini humo, baada ya kuzindua "sehemu ya kwanza" ya "mpango" kuondoamarufuku ya kutotoka nje uliowekwa kudhibiti maambukizi ya corona.
Waziri mkuu atajibu maswali kutoka kwa wabunge leo Jumatatu ambapo ofisi yake itachapisha muongozo ramsimi wa kurasa 50 na kuwasilisha bungeni.
Mwanasiasa wa chama cha Labour Sir Keir Starmer amekosoa mpango huo wa Waziri Mkuu kwa kukosa maelezo ya kina
Hayo yanajiri baada ya Scotland na Wales kupinga nembo ya ofisi ya Waziri Mkuu inayofahamika kama kaa chonjo "stay alert".
Siku ya Jumapili katika hotuba aliyoytangaza kwa njia ya televisheni kwa taifa, Bwana Johnson ''alitangaza mpango wa hali'', wa kufungua shughuli za kijamii, kuwaruhusu watu wa England, kufanya shughuli zao nje ya makazi yao kwa muda zaidi kuanzai Jumatano.
Waziri Mkuu alisema kuwa watu wanaweza kutofanyia kazi nyumbani- mkiwemo wale wanaofanyakazi viwandani- wanapaswa kurejea katika maeneo yao ya kazi, lakini waepuke usafiri wa umma.
Bwana Johnson alisema kuwa serikali ''itafanyjia marekebisho'' hatua za tatu za amri ya kukaa nyumbani kwa ''uangalifu'' hadi mwezi wa Julai.
Mfumo mpya wa kutambua virusi vya corona- Covid Alert System wenye hatua tano utasaidia haraka kufahamu ni kwa kiasi kgani amri ya kukaa nyumbani ambayo iliwekwa nchini Uingerezatarehe 23 Machi unaweza kubadilishwa.
Hatua ya kwanza itawaruhusu kuhfanya azoezi ya mwili nje au katika bustani na kucheza michezo baina ya watu wa familia mioja kuanzia Jumatano.
Mabadiliko katika miongozo yatawaruhusu watu kutoka katika nyumba tofauti kukutana katika maeneo ya kufanyia mazoezi iwapo watakaa umbali wa mita.
Anatumai hatua ya pili - "inayotarajiwa kuanza tarehe 1 Juni" - amesema kunaweza kufunguliwa terna kwa maduka na shule za baadhi ya wanafunzi wakubwa wa shule za msingi wanaweza kurudi shuleni.
Hatua ya tatu inaweza kuwezesha baadhi ya biashara za kitalii zikifunguliwa tena - "kama idadi itaturuhusu kama " - lakini sio mapema zaidi ya Julai 1. Waziri Mkuu huyo amesisistiza kuwa yote hayo yatawezekana kama "hali " itaruhusu, na kama haitaruhusu hatasita "kuweka breki " kama kutakua na milipuko mingine zaidi ya virusi vya corona.
Bwana Johnson kuhutubia Bunge Jumatatu, huku taarifa zaidi kuhusu mfumo wa utambuzi wa Covid-19 , matumizi ya barakoa, na kurejea kwa soka ya kulipwa.
Lakini Sir Keir alisema kuwa hotuba ya Bwana Johnson " imeibua maswali kuliko ilivyo yajibu".
Chanzo cha Habari BBC News.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.