Habari za Punde

Mwanachama wa Kumi wa CCM Achukuwa Fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Leo.19-6-2020

Kada wa Chama Cha Mapinduzi  Waziri wa Maji wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Prof. Makame M. Mbarawa (MB) akionesha Mkoba wa Fomu za Kugombea Urais wa Zanzibar baada ya kukabidhiwa na Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar kulia Ndg. Galosi Nyimbo, hafla hiyo imefanyika leo Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar. Profesa Mbarawa akiwa Mwanachama wa CCM wa 1O kujitokeza kuchukua fomu leo.
Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galos Nyimbo akimkabidhi moja ya fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Mwanachama wa CCM Profesa Makame Mbarawa alipofika katika Afisi za CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar kuchukua fomu za kuwania Urais kupitia CCM 
KATIBU wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar Ndg. Galosi Nyimbo akimkabidhi Fomu za kugombea Urais wa Zanzibar Prof. Makame Mbarawa, alipofika leo kuchukuwa fomu kuwania nafasi hiyo kupitia CCM.
Mgombea Urais wa Zanzibar Prof. Makame Mbarawa akikabidhiwa baadhi ya fomu za kugombea nafasi ya Urais na Katibu wa Idara ya Oganizesheni ya CCM Zanzibar.  f
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Prof. Makame Mbarawa akitoka katika jengo la Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar baada ya kuchukua fomu na kuelekea sehemu iliyoandaliwa kwa ajili ya kuzungumza na Waandishi wa habari Zanzibar.
Prof.Makame Mbarawa akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali walioko katika viwanja vya Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Jijini Zanzibar, baada ya kukamilisha zoezi la uchukuaji wa Fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar.
Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia maelezo ya mgombea Urais wa Zanzibar kupitia CCM Prof. Makame Mbarawa. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.