Habari za Punde

Tamwa yakutana kujadili utendaji kazi wa shughuli mwezi Januari hadi Juni 2020

 Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar Dkt,Mzuri Issa akifafanua jambo katika mkutano maalumu wa kujadili ripoti za utendaji kazi kwa Chama hicho kutoka mwezi Januari hani Juni.
 Afisa utafiti na ufuatiliaji TAMWA-Zanzibar Muhammed Khatib akiwasilisha moja ya ripoti za kiuendaji kwa taasisi hio kutoka mwezi Januari hadi Juni ambapo lengo kuu ni kuongeza kasi za utendaji katika shughuli za kila siku.
 Baadhi ya watendaji kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar wakifuatilia kwa umakini uwasiliswaji wa ripoti za kiutendaji kwa miezi sita kutoka mwezi Januari hadi Juni ambapo mkutano huo umefanyika kwa muda wa siku mbili.

Badhi ya watendaji kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA-Zanzibar wakifuatilia kwa umakini uwasiliswaji wa ripoti za kiutendaji kwa miezi sita kutoka mwezi Januari hadi Juni ambapo mkutano

huo umefanyika kwa muda wa siku mbili.



Muhammed Khamis,TAMWA-Zanzibar.


Watendaji wa Chama cha Waandishi wa habari Wanawake TAMWA-Zanzibar wamekutana na kujadili utendaji kazi wa shughuli mbali mbali kwa Chama hicho kwa muda wa miezi sita kutoka mwezi Januari hadi Juni mwaka huu.

Mkutano huo wa siku mbili ulifanyika  katika ukumni wa chama hicho uliopo Tunguu wilaya ya kati Unguja ambapo pia umewakutanisha watendaji kutoka ofisi za Pemba.

Awali Mkurugenzi wa Chama hicho Zanzibar Dkt,Mzuri Issa amewataka watendaji hao kuhakikisha wanaendeleza kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa.

Alisema ufanyaji kazi kwa bidii ndio nguzo kuu ya kuiasaidia jamii katika maeneo mbali mbali ya Unguja na Pemba hususani haki za wanawake na watoto.

Aliwataka wafanyakazi hao kufahamu kuwa jamii inakabiliwa na changamoto mbali mbali hivyo wafanyakazi hao wanapaswa kutambua kuwa wana wajibu mkubwa kwa jamii.

Miongoni mwa wafanyakazi hao walisema kufanyika kwa mkutano huo wa siku mbili kutaongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi z akila siku.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.