Habari za Punde

Ligi ya Mpira wa Kikapu Ikiendelea kwa Michezo Yake

NA MWANDISHI WETU
LIGI Kuu ya Zanzibar ya mpira wa Kikapu inazidi kuchanja mbuga katika uwanja wa Mao Dze Tung ambapo Usolo ilipokea kichapo cha kufungwa pointi 70-61 na Beit-el ras.

Ushindi wa timu hiyo unanifanya kuvuka nafasi moja kutoka wa sita mpaka saba na kuwashusha Usolo ambao nao watakuwa nafasi ya tano wakiwa na pointi sita pia.
Katika mchezo huo miamba hiyo ulionesha ushindani mkali hasa katika robo ya kwanza ambayo ilimalizika kwa kupitana na kwa pointi moja.

Beit el ras katika robo hiyo ikipata pointi 14 na Usolo ikajipatia pointi 13 ambapo hadi mapumziko iliongoza Beit el ras kwa pointi 21-10.

Robo ya tatu ya mchezo huo ilianza na miamba hiyo kuendelea kushambuliana na ilimalizika kwa Beit el ras kuongoza kwa pointi 20-17.

Katika robo ya nne ambayo ni ya lala salama Usolo ilionekena kuamka kwa kuishinda Beit el ras ambayo waliibuka na pointi 25-15 lakini kuongoza kwao hakukuweza kubadilisha matokeo ya mchezo huo kwa wapinzani wao ambao waliondoka na ushindi.

Beit el ras katika mchezo huo mchezaji wao  aliepata pointi nyingi za kufunga ni Abdul-azizi Mohammed ambae alipata pointi 14 na katika timu ya Usolo ni Salum Bakari ambae alipata pointi 13.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.