Habari za Punde

Mtendaji Mkuu wa TARURA Atembelea Miradi ya Barabara Rukwa


Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff (aliyevaa kofia) akiangalia eneo linapojengwa Daraja la Kavunja linalounganisha Kata ya Kirando na Korongwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa. 


Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff (aliyevaa kofia) akikagua ujenzi wa barabara za Mjini-Matai kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Km 1 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.


Mtendaji Mkuu wa TARURA, Mhandisi Victor Seff (aliyevaa kofia) akikagua sehemu iliyokamilika ya ujenzi wa barabara za Mjini-Matai kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Km 1 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa.
Na. Geofrey A.Kazaula
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),Mhandisi Victor Seff amemtaka Mkandarasi ambaye ni Mbuya’s Contractors Company Limited anayejenga Barabara za Mjini-Matai katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa kukamilisha mradi unaotokana na Ahadi za Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Magufuli kwa muda kulingana na mkataba.

Mtendaji Mkuu amemuelekeza Mkandarasi huyo kuhakikisha anazingatia viwango katika kutekeleza mkataba huo ili barabara ziweze kuwa na ubora unaotakiwa.

‘‘Unatakiwa kuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati lakini pia unazingatia viwango vinavyotakiwa, na mimi mwenyewe nitarudi hapa kujiridhisha’’ alisema Kiongozi huyo.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Seff alitembelea miradi ya barabara na madaraja katika Halmashauri mbalimbali ndani ya Mkoa wa Rukwa ambapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi alitembelea miradi ya barabara za lami katika Mji wa Namanyere zilizokamilika na zinazoendelea kujengwa kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

Aidha, Mtendaji Mkuu wa TARURA alitembelea na kujionea hali ya Daraja la Kavu lililopo Kijiji cha Kirando katika Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa ambapo hakuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo na jinsi ambavyo Ofisi ya Mratibu wa Mkoa wa Rukwa inavyoshughulikia changamoto zilizojitokeza za menejimenti ya mkataba na usanifu wa daraja hilo. 

Hivyo, aliahidi kutuma Timu ya Wataalam kuja kwenye daraja hilo na kutoa mapendekezo ya jinsi ya kutatua changamoto hizo.

Akiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, Kiongozi huyo alitembelea na kujionea hali ya daraja la Kankwale lililopo Kata ya Kankwale ambalo pia limeharibika kutokana na mvua nyingi zilizonyesha na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ambapo aliagiza kuwa ujenzi wa daraja hilo unanza mara moja kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ili kuhakikisha huduma za usafiri na usafirishaji zinarejeshwa kwa wananchi.

Naye Kaimu Mratibu wa TARURA Mkoa wa Rukwa, Mhandisi Selemani Mziray amesema kuwa katika Mji wa Namanyere, ujenzi wa barabara za lami zinazotokana na Ahadi za Mhe. Rais, hadi sasa kilo mita mbili (2) zimekamilika na kilo mita moja (1) ipo katika utekelezaji na itakamilika tarehe 30/08/2020.

‘‘Tunajitahidi ili kuhakikisha miradi hii inayotokana na Ahadi za Mhe. Rais inakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyotakiwa ili wananchi waweze kunufaika”, alisema Mhandisi Mziray.

KablayakuhitimishaziarayakemkoaniRukwa, MtendajiMkuuwaTARURA alifanyakikaokazinaMamenejawotewa TARURA waliopokwenyeHalmashaurizotezilizopokwenyeMkoawaRukwailikutoamaelekezombalimbaliikiwanipamojanakujadilinamnayakuendeleakurejeshamawasilianokwamaeneoyaliyoathiriwasananamvua.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.