Habari za Punde

WAGOMBEA WATAKIWA KURANGAZA SERA SIYO RASILIMALI ZA NCHI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Luhaga Mpina akizungumza na wachuuzi wa samaki katika soko la samaki la Deep-sea jijini Tanga jana alipotembelea na kuzungumza na wavuvi na wachuuzi  wa Soko hilo.
PICHA NA HAMIDA KAMCHALLA


Na Hamida Kamchalla, TANGA.
WANASIASA wanaogombea nafasi mbalimbali za uongozi wametakiwa kuyatumia majukwaa yao kueleza sera zao na siyo kutumia nafasi hizo kueneza dhana potofu zinazogusa rasilimali za nchi zilizopo kisheria kama suala la kuruhusu uvuvi haramu.

Akiongea na wavuvi pamoja na wananchi jijini Tanga katika soko la samaki la Deep-sea Waziri wa Uvuvi na ufugaji Mhe.Luhaga Mpina alisema kuwa wapo watu wanaogombea nafasi za uongozi wakitumia kero za wananchi ambazo nyingine zinalindwa na sheria ya nchi.

Mpina alibainisha kwamba suala la wavuvi kufanya shuhuli za Uvuvi haramu limepingwa kisheria na endapo wataendelea kufanya hivyo sheria zitafuata mkondo na kuwakamata wahusika ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua Kali na kuwachomea nyavu zao.

"Wito wangu kwa wavuvi na wananchi wote kwa ujumla wanaogombea nafasi za uongozi, watakaotumia fursa hiyo kuingilia rasilimali za nchi watachukuliwa hatua kali, kama wapo majukwaani watashushwa na watapelekwa mahakamani, rasilimali hizi ni lazima zilindwe wakati wote" alisema.

Aidha aliwataka wavuvi hao kufuata sheria zilizopo ili kuvua samaki kwa Uhuru na uhalali kwani watakapofanya uvuvi haramu sio tu kuchukuliwa hatua bali pia wanahatarisha maisha ya viumbe wengine vilivyopo baharini vikiwemo ambavyo ni chakula cha samaki.

Kwa upande wake Pascal Mbui ambaye ni mvuvi katika Bahati ya Deep-sea aliiomba serikali kuboresha sheria za uvuvi na kuziweka wazi ili wapate i zao kuzitambua kwani wamekuwa wakitozwa faini ambazo hawazielewi kulingana na makosa wanayotajiwa kwenye shuhuli zao.

"Wavuvi wadogo wadogo tuko nyuma sana kuzielewa hizo sheria, tunaiomba serikali ituboreshee na kutuhamasisha kuhusu uvuvi wa kisasa ili nasisi tuweze kutunza mazingira ya baharini, na hizo sheria ziainishwe na kuwekwa wazi ili tuzielewe kulingana na makosa hata ukitozwa faini unaelewa kosa lako" alisisitiza.

Hata hivyo wavuvi na wachuuzi hao wameiomba serikali kuwapatia mikopo itakayowawezesha kununua zana za kisasa za kuvulia huku wakiomba kuendelea kutumia majenereta wakati wa usiku kwenye uvuvi baada ya kuzuiliwa kuyatumia kutokana na kilichoelezwa kuwa yana mwanga mkali ambazo unaleta athari ndani ya bahari.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi (TADB) Japhet Justin alisema kuwa lengo la wao kuwatembelea wavuvi hao ni kuona jinsi ya kuwasaidia kuwapatia mikopo ili waweze kuendesha shuhuli zao kwa tija.

Justin alitoa hamasa kwa wavuvi hao kujiunga kwenye vikundi vya ushirika ili wapatiwe mikopo na kuongeza kuwa watakaopewa kipaumbele katika mikopo hiyo ni wale ambazo tayari wameshajiunga kikundi ndipo waangalie jinsi ya kutoka mikopo kwa mtu mmoja mmoja.

"Wavuvi mnakopesheka, zamani watu walikuwa na dhana kwamba wavuvi hawakopesheki lakini siai uwezo wa kumikopesha tunao lakini ni kwenye ushirika wenu, wote tutamioatia mikopo lakini wa kwanza kupata nafasi hii ni wale watakaokuwa kwenye ushirika, kuwepo kwenu nyinyi hapa kwenye mwalo huu kunatupa sisi fursa ya kuwakopesha tena kwa riba nafuu sana" alifafanua.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.