Habari za Punde

Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Ramia Atembelea Kiwanda Cha Mafuta ya Majani Makavu ya Mkarafuu Mgelema Chakechake Pemba.

WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Mohammed Ramia Abdiwawa, akipata maelezo juu ya kifaa maalumu kinachoonyesha uwepo wa mafuta ya majani ya Mkarafuu baada ya kukamuliwa, kutoka kwa Katibu wa kikundi cha TUNAWEZA Suleiman Habibu Issa huko Mgelema Wilaya ya Chake Chake, wakati ziara yake hivi karibuni
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa, akiangalia kinu maalumu kinachokamulia majani makavu ya Mkarafuu huko Mgelema Wilaya ya Chake Chake.
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa, akimsikiliza kwa makini Mdhamini wa ZSTC Pemba Abdalla Ali Ussi (katikati), wakati alipokuwa akitoa maelezo juu ya ufanyaji kazi wakiwanda cha kukamulia majani makavu ya Mkarafuu huko Mgelema Wilaya ya Chake Chake
WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa, akiteremka kutoka juu ya kiwanda cha kukamulia majani makavu ya Mkarafuu, baada ya kukagua kiwanda hicho huko Mgelema Wilaya ya Chake Chake

WAZIRI wa Fedha na Mipango Zanzibar Balozi Mohamed Ramia Abdiwawa, akimsikiliza Mdhamini wa ZSTC Pemba Abdalla Ali Ussi, juu ya uwepo wa majani makavu ya mkarafuu yanayokamuliwa mafuta huko Mgelema Wilaya ya Chake Chake.
(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.