Habari za Punde

Mwenyekiti wa CCM Taifa Aongoza Kikao cha NEC Jijini Dodoma leo.


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza wakati akifungua Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, kilichofanyika katika ukumbi wa White House Jijini Dodoma leo.20/8/2020.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli amewasihi Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kujadili mapendekezo ya wagombea kwa kuweka mbele maslahi ya Chama na Taifa kwa jumla kwani wanaCCM na Watazania wanaimani kubwa  na chama hicho.

Wito huo ameutoa leo katika Mkutano Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa CCM (White House), Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa chama hicho akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia, ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais Magufuli alitoa wito huo wa kujadili mapendekezo kwa umakini mkubwa kwa kumtanguliza Mwenyezi Mungu mbele na kuyatuanguliza mbele maslahi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Taifa na kutoweka mbele udugu, urafiki, ukanda ama dini bali uwezo wa mtu uongoze.
Alisema kuwa hivyo ndivyo walivyofunzwa na waasisi wa chama hicho Hayati Mzee Abeid Amani karume na Hayati Mwalimu Julius Nyerere na huo ndio msingi uliopelekea chama hicho kuendelea kuaminiwa na wananchi tokea nchi hiyo kupata uhuru.

Aliwashukuru wajumbe wa NEC kwa kumpigia kura nyingi na pale walipokwenda katika maeneeo yao walishiriki wka akiasi kikubwa katika kumtafutia wadhamini ambapo alipata wadhamini zaidi ya Milioni 1.1 huku akisema kuwa alipata wadhamini wengi sana katika Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

Alisema kuwa mkutano huo ulikuwa na ajenda moja kubwa wa kufanya yteuzi wa kugombea Ugunbe na Uwakilishi, ambapo mchakato wake ulizna mwezi mmoja uliopita ambapo wajumbe walipiga kura na kupendekeza majina na baada ya kupitia ngazia mbalzai mbali waliwepza kufika katika kikao hicho.

Aliwapongeza wagombea wote wa CCM waliojitikeza kugombea nafasi mbali mbali kwani walikuwa ni wengi sana hiyo ni kutokana na kuwa chama hicho kinapendwa.

Alieleza kuwa wagobea walikuwa ni wengi sana wakiwemo wafanyakazi, akinamama , wasomo, akibababa, viongozi wa NGOs, wavuvui na walemavu wote waliomba CCM, hiyo ni kusipitishwa kuwa CCM inapenwa sana.

Alisema kuwa hapana chama waliojitokeza Wagombea wengi hatua ambayo inayonesha ni kuvunja rekodi katika bara la Afrika kuwa ni chama kinachopendwa na kinachoheshimika na kikubwa chenye mtandao mkubwa katika kuleta ushindi.

Rais Dk. Mgufuli alisema kuwa hayo ni matokea makubwa na kazi nzuri katika  kusimamia chama na Serikali katika utekelezaji wa Ilani, ambapo katika miaka mitano wajumbe hao wamekuwa wakitembelea miradi mbali mbali na kutoa maelekezo pamoja na kukemea kwa wale waliozembea, ambapo miradi mingi imeweza kukamilika katika Majimbo yao.

“Huu ni ushahidi kwamba Wajumbe wa NEC wamesimamia Chama na Utekelezaji wa Ilani ya CCM……….Hayo ni matunda mazuri ya uchapakazi wenu na ndio maana mkaona watu wengi wamejitokeza katika kugombea nafasi mbali mbali kupitia CCM”, alisema Dk. Magufuli.

Alisema kuwa vikao vilivyopita vilijadili vizuri sana ndani ya siku mbili na kufanya uchambuzi wa kina ambapo walitumia vianzio vingi na kuwahakikishia wajumbe kwua ameseoma majina yote 10367.

Alieleza kuwa hawakumpendelea mtu ama kumnyima mtu haki yake na badala yake walitumia taarifa nyingi na kuwajadili wagombea kwa muda mrefu ili watakaopitishwa wawe watu wenye uwezo wa kuipeperusha vyema bendera ya CCM na hatimae kuleta ushindi na kukipelekea chama hicho kuendelea kuongoza nchi.

Aliongeza kuwa kulikuwa na haja ya kufanya uchambuzi wa kina kwani unyeti wa nafasi zinazogombewa za Ubunge na Uwakilishi ni nyeti na muhimu sana kwani hao ni wasemaji wa wananchi kwani pia, wanajukumu na kusimamia Serikali, hivyo ilikuwa ipo haja ya kufanywa mchakato huo mkubwa.

Alisema kuwa kwani ndani ya Wabunge na Wawakilishi ndimo anakapopatikana Waziri Mkuu, Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mawaziri na Manaibu Waziri, Spika, Naibu Spika na Wenyeviti  wa Bunge na Baraza la Wawakilishi.

Hivyo, Mwenyekiti huyo wa CCM alisema kuwa ni vyema kuwajadili kwa dhati kabisa kwani ili kudhiridhisha kuwa wale watakaopitishwa wana sifa zinazostahili kuwa viongozi na wanaofahamu Dira za nchi na Sera za CCM.

Rais Magufuli aliwashukuru Wajumbe wa Kamati Kuu kwa kazi nzuri walizofanya siku mbili ambayo imerahisisha kufanya shughuli hiyo na kusema kuwa Kamati ya Usalama na Maadili na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu zimejitahidi kuchambua na kupata wagombea wawenye sifa zinazokubalika zikiwemo kuwa wazalendo, kujitoa kwenye chama, wenye utayari kuwatumikia wananchi na Watanzania wote na ambao wanokubalika na wananchi.

Alisema kuwa baada ya mchakato uliofanyika kuanzia ngazi ya Jimbo hadi Kamati Kuu na kueleza kuwa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM ndiyo iliyopewa jukumu la mwisho la kufanya uteuzi wa mwisho wa Ubunge na Uwakilishi.

Mapema Katibu Mkuu wa CCM Bashiru Ali Kakurwa alisema kuwa kikao hicho hakitajadili nafasi za Uwakilishi na badala yake kitafanya zoezi hilo  kwa nafasi ya Ubunge pekee.

Aliongeza kuwa watakaoteuliwa na kikao hicho ndio watakaopata nafasi ya kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.