Habari za Punde

Wakaazi wa kijiji cha Dundua wapongezwa kwa kuhama kupisha mradi wa uwekezaji wa gesi na mafuta

Na Mwandishi wetu


MKUU wa Wilaya ya Kaskazini B Rajab Ali Rajab amewapongeza wakaazi wa kijiji cha Dundua kwa kukubali kuhama katika maeneo yao kwa ajili ya kupisha uekezaji wa mradi wa gesi na mafuta katika ukanda wa Bumbwini.

Alisema  kitendo hicho kimeonesha wazi jinsi wananchi hao walivyoungana na serikali  katika jitihada za kupeleka maendeleo kwa wananchi wake kupitia mradi huo

Akizungumza  katika zoezi la upandaji wa miti katika nyumba mpya zilizojengwa na serikali kwa ajili ya fidia ya wananchi hao  huko dundua ikiwa ni matayarisho ya mwisho ili nyumba hizo ziweze kukabidhiwa rasmi na mh;raisi dk ali muhammed shein hivi karibuni

Mkuu huyo wa wilaya amesema  serikali imeamua kujenga nyumba bora kwa ajili ya kulipa  hisani kwa wananchi wake

Hata hivyo alizipongeza taasisi zote  ambazo zimeshiriki kwa kiasi kikubwa ikiwemo wasimamizi wa mradi huo zura , wakala wa ujenzi zba, pamoja na idara maalumu za smz kwa  ushirikiano wao waliouonesha mpaka kukamilika kwa ujenzi wa nyumba hizo.

Aidha aliwataka wananchi hao kuitunza miti iliyopandwa katika kijiji hicho ili iweze kukua na kuleta haiba nzuri katika kijiji hicho

Msaidizi  Mkurugenzi  Kilimo  Halmashauri ya Wilaya ya Aaskazini B Suleimani Khamisi Suleimani amesema  katika kijiji hicho wanatarajia kuanzisha kamati maalumu kwa ajili ya kushughulikia mazingira ya kijiji hicho ili kuweka kumbukumbu kwa kizazi kijacho.

Hata hivyo aliahidi kutoa mafunzo maalumu kwa wakaazi wa nyumba hizo ili waweze kukabiliana na mazingira ya nyumba hizo.

Akizungumza     kwa niaba ya wanakijiji hicho Azizi Shaibu Rajab kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Dundua wameishukuru serikali kwa hatua walioichukua ya kuwajengea nyumba bora na kuahidi kuzitunza  nyumba
hizo ili ziweze kudumu.

 Jumla  ya nyumba 31 zimejengwa na serikali kwa ajili ya kulipa fidia wakaazi wa kijiji cha Dundua ili kupisha uwekezaji wa gesi na mafuta.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.