Habari za Punde

ZEC Yatowa Mafunzo Kwa Wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar Unaotarajiwa Kufanyika Mwaka huu 2020.


Na.Mwandishi Wetu ZEC.

Wasimamizi na Wasaidizi wa Uchaguzi wa Wilaya wametakiwa kuwa waaminifu ,waadilifu,  na kuweka uzalendo mbele wakati wanapotekeza majukumu yao hatua ambayo itasaidia kufanikisha Uchaguzi mkuu wa Zanzibar unaotarajiwa kufanyika 28 Oktoba 2020

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC Mhe Jaji Mkuu Mstaaf wa Zanzibar.Mhe.Hamid Mahmoud akizungumza wakati akifunga mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi hao alisema matarajio ya Tume ni kuisimamia kazi ya Uchaguzi kwa kufuata taratibu na miongozo ambayo ndio chachu ya kupata maendeleo ili nchi kuendelea katika hali ya amani wakati wote.

Jaji Mkuu Mstaaf Mhe. Mahmoud amesema uchaguzi wa mwaka huu 2020 unafanyika kwa kuzingatia mabadiliko ya Sheria ambayo yamepelekea kutungwa kwa sheria namba 4 ya mwaka 2018 ambayo inamasharti mbalimbali mapya ya kufuatwa katika kuendesha uchaguzi.

Hivyo. Jaji Mkuu Mstaaf Mhe. Mahmoud aliwanasihi watendaji wa Tume na wadau wa uchaguzi watumie wakati wao mwingi kuisoma sheria hiyo na kanuni zake ili kupata mwanga mzuri katika kutekeleza majukumu yao.

Kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha uhasibu cha Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ndg. Talib Abdalla Salum, aliwashauri watendaji wa tume hiyo kuchukua tahadhari juu ya matumizi mabaya ya fedha za serikali na kujenga uwelewa zaidi wa kufanya marejesho baada ya matumizi

Mapema Hakimu wa Mahkama ya Mkoa Vuga Mhe.Khamisuu Sadun Makanjira aliwaapisha Wasimamizi hao ili kutekeleza majukumu yao kusimamia uchaguzi kwa uadilifu na utii kwa mujibu wa Katiba, Sheria, Kanuni za Miongozo ya Uchaguzi.

Wakielezea matarajio yao baada ya kupatiwa mafunzo washiriki wa mafunzo hayo waliahidi kuwa wako tayari kuyafanyiakazi kivitendo mafunzo waliyopatiwa na kuzitekeleza sheria za uchaguzi ili kuendelea kuweka nchi katika hali ya amani na utulivu hata baada ya Uchaguzi

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.