Habari za Punde

CCM MKOANI TANGA IMEJIPANGA KUTWAA USHINDI VITI VYOTE

Na Hamida Kamchalla, TANGA.
KATIBU wa Jumuiya ya Wazazi mkoani Tanga Lawrent Msuya amesema kuwa CCM Mkoani humo imejipanga kuhakikisha viti vyote kuanzia ngazi za kata hadi uraisi vinakwenda kwenye chama hicho ifikapo octoba 28 mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu.

Msuya aliyasema hayo jana ofisini kwake wakati akizungumzia hali ya uchaguzi mkoani humo na mikakati ya chama hicho ambapo alisema CCM Wana mbinu zote za uchaguzi hivyo hawawezi kupoteza nafasi hata moka kwenye majimbo na Kata.

Alieleza kwa "Hatuna mashaka na Mgombea uraisi Dkt. John Pombe Magufuli hii ni wazi atachukia kiti hicho ifikapo octoba 28 lakini tuna mkakati wa kutembea ngazi za chini kusaka kura za ubunge na madiwani na tuna uhakika viti vyote tunavichukua, ikitokea kupoteza labda udiwani tena pia ni kwa Bahati mbaya sana".

Msuya alibainisha kwamba tayari mkakati huo umeshaanza kufanyiwa kazi na maeneo yote yenye upinzani yamepewa kipaumbele kuyapambania kuhakikisha ushindi unapatikana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.