Habari za Punde

KATIBU MKUU DK.ALOYCE NZUKI AWAPONGEZA SAO HILL KUVUKA LENGO LA UKUSANYAJI WA MAPATO.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Aloyce Nzuki akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Shamba la miti la Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

 Na Fredy Mgunda,Mufindi.
 Katibu mkuu wa wizara ya Maliasili na Utalii amewapongeza TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill lililopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kwa kuvuka lengo la makusanya ya mapato ya mwaka.

Akizungu alipokuwa alipotembelea Shamba la Miti Sao Hill,Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dk.Aloyce Nzuki alisema kuwa ameona shughuli za upandaji miti za utunzaji  zinazofanywa na shamba .

Alisema kuwa anatoa pongezi hizo kwa TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill kwa kufaya kazi nzuri ambayo hupelekea taifa kunufaika kutokana na uwepo wa Shamba hili ambalo ni shamba kongwe na shamba kubwa kuliko mashamba yote ya miti ya kupandwa nchini.

"Mnafanya kazi nzuri sana,nimeona hapa kwenye taarifa yenu ,wakati wengine wamepata shida sana kipindi cha Covid lakini ninyi mmeweza kufanya biashara vizuri, nikiangalia jedwali ambalo Mhifadhi Mkuu amelisoma jedwali namba  tatu,naona hapa kwa ujumla miaka hiyo mitano iliyotajwa mmevuka lengo kwa asilimia kumi na mbili (12%) ambayo ni mafanikio mazuri sana"Alisema Dr. Aloyce Nzuki

"Lakini kwa mwaka ule 2018/2019 tayari mlikuwa mmeshavuka lengo kwa asilimia 28.7 (28.7) mlikuwa mko juu ya mapato yale ya nyuma yake,na mmeonesha mnauwezo mkubwa sana wa kufanya biashara yote inayohusiana na mazao ya misitu lakini pia ya mazao ya nyuki",Alisema Dr Nzuki
Aliendelea kusema kuwa kwa jitihada hizo TFS inastahili kupongezwa na kuwataka kuendelea  kuhamasishana watumishi wote kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza pato la taifa.

Aliwaeleza watumishi kuwa utekelezaji wa Ilani unategemea sana jitihada za watumishi walio na weredi,kujituma na uzalendo na hivyo eneo ambalo TFS inalisimamia ni maeneo ambayo yameelekezwa na viongozi ili kuchangia ukuaji wa pato la taifa.

"Niseme kitu kimoja majukumu ambayo yapo mbele yetu  ni kutokana na ilani ya Chama cha Mapinduzi kwamba eneo hili ambalo mnalisimamia ambalo linatokana mazao ya misitu na nyuki ni maeneo ambayo yametajwa na yameelekezwa na ilani yanayotarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa katika maendeleo ya taifa na mwananchi mmojammoja,”Dr Nzuki

Hata hivyo aliitaka TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill kuendelea kuweka ushirikiano mkubwa na jamii inayolizunguka shamba ili kuepuka majanga ambayo yanahatarisha usalama wa shamba na mali zilizomo ambayo yamekuwa yakijitokeza

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.