Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chakechake Pemba wakati wa Ufunguzi wa Kampeni za CCM Pemba kuwatambulisha Wagombea wake. na kumptambulisha Mgombea Urais wa Zanzibar Dk Hussein Mwinyi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein amewataka wanaCCM pamoja na wananchi kiswani Pemba kumchagua Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi kuwa Rais wa Zanzibar kwani ndie pekee anaeweza kuyalinda Mapinduzi ya Januari 12, 1964 pamoja na kuutunza Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Dk. Shein aliyasema hayo leo katika mkutano wa
uzinduzi wa Kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kisiwani Pemba, uliofanyika
katika viwanja vya Gomnani ya Kale, Chake Chake Pemba katika Mkoa wa Kusini
Pemba ambao ulihudhuriwa na mamia ya wanaCCM.
Katika maelezo yake, Makamo Mwenyekiti huyo wa CCM
Zanzibar alisema kuwa
Dk. Hussein Mwinyi ndie pekee anaeweza kuyalinda
na kuyatunza Mapindzi ya Januari 12.1964 pamoja na Muungano wa Tanganyika na
Zanzibar na hakuna kiongozi mwengine anaeweza kutekeleza hayo miongoni mwa wale
wanaogombea nafasi hiyo.
Makamao Mwenyekiti
huyo wa CCM alieleza kuwa Zanzibar imepata uhuru wake kupitia Mapinduzi
Matukufu yaliyofanyika mwaka 1964 ambapo kipindi chote hicho hadi hivi leo CCM
ndio inayoongoza dola hivyo, chama hicho kinatambua mahitaji na maisha ya
wananchi hasa wanyonge.
Rais Dk. Shein alisema kuwa Dk. Hussein Mwinyi
anaiweza kazi ya kuyalida Mapinduzi na kuuimarisha Muungano kwani ameshaifanya
kwa kipindi kirefu kupitia nafasi za uongozi alizoitumikia ndani ya Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa kwa kipindi kirefu sambamba na kuwa Waziri katika Ofisi ya Makamo
wa Rais anayeshughulikia masuala ya Muungano.
Aidha, Makamo huyo Mwenyekiti wa CCM alisema kuwa siku
zote chama hicho hakibahatishi kuwachagua viongozi wake katika nafasi za Urais
na ndio maana katika chaguzi zote wamekuwa wakipata ushindi mkubwa, hivyo
kuchaguliwa kwa Dk. Hussein Mwinyi kunaonesha wazi usshindi w akishindo kwa CCM
unakuja.
Rais Dk. Shein alisema kuwa CCM imemchagua Dk.
Hussein Mwinyi kuwa mgombea nafasi ya Urais kutokana na sifa zote za kuwa Rais
hasa ikizingatiwa kuwa yeye anapenda haki na anaichukua rushwa kwani ni mtu
safi.
Pia, Rais Dk. Shein alisema kuwa Dk. Hussein
Mwinyi ni mtu mwenye maadili na kiongozi mchapa kazi mahiri na mwenye elimu
kubwa na mwenye utaalamu wa afya na
aliyebobea katika fani hiyo kwani ni mtu anayejituma sana.
Rais Dk. Shein alisema kuwa yeye mwenyewe binafsi
anamfahamu sana Dk. Hussein Mwinyi kutokana na kuwa ameshawahi kufanya nae kazi
wakati Rais Dk. Shein akiwa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
na Dk. Hussein Miwnyi akiwa Waziri katika Ofisi hiyo anayeshughulikia Muungano.
Aliongeza kuwa Dk. Hussein Mwinyi ni kiongozi
mwenye maadili, heshima na nidhamu ya hali ya juu na hawezi kufananishwa na
wagombea wengine wa nafasi hiyo ya Urais wa Zanzibar.
“Dk. Hussein ataongoza ushindi wa CCM kwani
aliyepewa kapewa na wala hapokonyeki kwnai uwezo wake mkubwa sana”alisisitiza
Makamo Mwenyekiti huyo wa CCM Zanzibar.
Hivyo, Rais Dk. Shein aliwataka wananchi wa kisiwa
cha Pemba kutokubali kubabaishwa wala kulazimishwa kumchagua mtu asie kuwa na
sifa za kuiongoza Zanzibar na badala yake wamchague kiongozi kutoka CCM.
Aidha, Rais Dk. Shein alieleza matumaini yake
makubwa aliyonayo kwa Dk. Hussein Mwinyi katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi mpya
ya mwaka 2020-2025 kama alivyosimamia yeye Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010-2015
na ile ya 2015-2020.
Makamo Mwenyekiti huyo alitumia fursa hiyo
kumuombea kura Dk. Hussein Mwinyi pamoja na
wagombea wengine wote wa CCM wa kisiwani Pemba huku akitumia fursa hiyo
kuwanadi wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa CCM wa Mikoa Miwili ya Pemba
pamoja na kuwakabidhi Ilani ya chama hicho ili waende wakainadi kwa wananchi.
Rajab Mkasaba, Ikulu
Zanzibar
Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax:
024 2231822
E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk
No comments:
Post a Comment