Habari za Punde

Kikundi cha Mazoezi ya Viungo Zanzibar Cha Pressure Group Pangawe Champongeza Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe Dk Hussein Mwinyi.

 Mwenyekiti wa Pressure Group Pangawe Nd. Abdullah Seif  Makame amempongeza Mgombea wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi Dr. Hussein Ali Mwinyi kwa kudhamiria kujenga Bandari ya Kizimkazi endapo atapewa ridhaa na Wananchi wa Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu.

Nd. Abdullah amesema kuwa ahadi ya Mgombea huyo ya kujenga Bandari Kizimkazi aliyoitoa  katika Mkutano wake wa Kampeni  huko Makunduchi imewakuna Wananchi wote wa Mkoa wa Kusini kwani hicho ni kilio chao cha siku nyingi.

Amesema Bandari ya Kizimkazi itawakomboa Kiuchumi Wananchi mbali mbali wa Mkoa wa Kusini pamoja na ile jirani kwa vile uwepo wake utawarahisishia  usafiri wa kupeleka na kuingiza kutoka sehemu mbali mbali ikiwemo Bandari ya Dar es salaam.

Mwenyekiti huyo wa Pressure Group amesema agenda ya Mgombea huyo wa Urais wa Zanzibar Dr. Mwinyi imewashawishi Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja kubashiri kwamba Kiongozi huyo ndie anayestahiki kuwa Rais wa Zanzibar wa Awamu ya Nane.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.