Habari za Punde

Maalim Seif amepiga kura leo kituo cha Garagara jimbo la Mwera

 

MGOMBEA urais Zanzibar kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Maalim Seif Sharif,  amefika katika kituo cha Garagara, Jimbo la Mwera,  na kupiga kura mapema leo Jumatano, Oktoba 28, 2020.

Mgombea Urais kwa tioketi ya ACT- Wazalendo Maalim Seif Sharif Hamad akiongea na waandishi wa habari baada ya kumaliza kupiga kura yake leo ambapo amesema  ametiwa moyo na watu wengi kujitokeza katika vituo vya kupigia kura ila amegundua wananchi wengi wana malalamiko ya kutokuona majina yao kwenye vituo walivyojiandikisha.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.