Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein Ajumuika na Wananchi wa Jimbo la Tunguu Katika Zoezi y la Upigaji Kura Kituo cha Bungi leo.28/10/2020.1

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein  wa tatu akiwa katika foleni akisubiri zamu yake kwa ajili ya upigaji wa kura katika Kituo cha kupigia Kura Skuli ya Bungi Wilaya ya Kati Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, akiwa katika foleni akisubiri zamu yake kwa ajili ya kupiga kura yake kuwachagua Rais wa Zanzibar,Rais wa Tanzania  Mbunge.Mwakilishi na Diwani , akiwa katika Kituo cha Kupigia Kura Skuli ya Bungi Wilaya ya Kati Unguja.leo 28/10/2020.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein  akielekezwa sehemu ya kupigia kura baada ya kukabidhiwa kura yake na Mkuu wa Kituo cha Wapigaji kura Skuli ya Bungi Ndg.Khamis Ali Juma, wakati wa zoezi la upigaji kura lililoaza leo Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika Kituo cha Kupiga kura Skuli ya Bungi Wilaya ya Kati Unguja, akiangaliwa jina lake katika Daftari la Mpiga kura na Mkuu wa Kituo cha kupiga kura Ndg. Khamis Ali Juma, wakati wa zoezi la upigaji kura lililofanyika leo 28/10/2020.
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akipiga kura yake leo katika Kituo cha kupigia kura Skuli ya Bungi Wilaya ya Kati Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akipiga kura yake kumchagua Rais wa Tanzania, Rais wa Zanzibar, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani, zoezi la upigaji kura lemefanyika leo katika Kituo cha Kupigia Kura Skuli ya Bungi Wilaya ya Kati Unguja leo.
.RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar baada ya kumaliza zoezi la upigaji kura leo,28-10-2020, katika Kituo cha Upigaji Kura Skuli ya Bungi Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.