MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC
Taifa Hamad Rashid Mohamed, akitumbukiza kura yake katika moja ya masanduku ya
kura yaliyowekwa na tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC, katika kituo cha kupigia
kura Fidel Casro Wawi jimbo la Wawi.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha ADC
Taifa Hamad Rashid Mohamed, akitumbukiza kura yake katika moja ya masanduku ya
kura yaliyowekwa na tume ya uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania NEC,
katika kituo cha kupigia kura Fidel Casro Wawi jimbo la Wawi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi
CUF Mussa Haji Kombo, akitumbukiza kura yake katika moja ya masanduku ya
kupigia kura yaliyowekwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC)katika kituo cha
Wara kilimo Mchaomanne jimbo la Wawi. (PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha wananchi
CUF Mussa Haji Kombo, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo mbali
mbali vya habari Tanzania, mara baada ya kupiga kura kituo cha Wara kilimo
Mchaomanne jimbo la Wawi.(PICHA NA ABDI
SULEIMAN, PEMBA)
BAADHI ya wananchi wa jimbo Wawi Wilaya ya Chake
Chake, wakitumbukiza karatasi zao za kupigia kura baada ya kuchagua kiongozi
anaye mtaka, katika kituo cha kupigia kura wawi B jimbo la Wawi.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha Wakulima
Tanzania (AFP) Said Soud Said, akizungumza na waandishi wa habari kutoka vyombo
mbali mbali vya habari Tanzania, mara baada ya kupiga kura kituo cha Skuli ya Wawi
Jimbo la Wawi Wilaya ya Chake Chake.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
BAADHI ya akinamama wa jimbo la kojani Wilaya ya
Wete wakiwa katika foleni kusubiri kupiga kura katika kituo cha kupigia kura
skuli ya Kangagani Jimbo la Kojani Wilaya ya Wete.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha NRA
Zanzibar Khamis Faki Mgau, akitumbukiza kura yake katika moja ya masanduku
yaliyowekwa na Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) katika moja ya vituo vya kupigia
kura skuli ya Kangagani jimbo la Kojani.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kupitia chama cha NRA Taifa Khamis Ali Hassan, akitumbukiza karatasi
yake ya kupigia kura katika moja ya masanduku ya upigaji wakura yaliyowekwa na
Tume ya Uchaguzi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika moja ya vituo vya
kupigia kura skuli ya Kangagani jimbo la Kojani.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
MGOMBEA Urais wa Zanzibar kupitia chama cha AFP Said
Soud Said, akitumbukiza karatasi yake ya kupigia kura katika sanduku maalumu la
kupigia kura lililowekwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kituo cha kupigia
kura Skuli ya Wawi jimbo la Wawi.(PICHA
NA ABDI SULEIMAN, PEMBA)
No comments:
Post a Comment