Habari za Punde

Majaliwa : Shilingi Bilioni Saba Zimetolewa Kwa Ujenzi wa Miradi ya Maji Lushoto.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa  akizungumza na wananchi wa Lushoto wakati alipowaomba wampigie kura mgombea  Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli,
Wananchi wa Lushoto  wakimsikiliza, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati alipomuombea kura mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli.
Wananchi wa Lushoto  wakimsikiliza, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Kassim Majaliwa wakati alipomuombea kura mgombea Urais wa CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, Oktoba 9, 2020. 

MJUMBE wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amesema Serikali imetoa shilingi bilioni 7.784 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Lushoto, Tanga.

Ameitaja miradi hiyo kuwa ni ujenzi wa mradi wa maji Mgwashi (bilioni 1.570), mradi wa maji Mlola/Lwandai (milioni 412), ujenzi wa mradi wa maji IIrente (milioni 195), mradi wa maji Soni/Mkuzu (milioni 490) ambayo imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi.

Ameyasema hayo leo (Ijumaa, Oktoba 9, 2020) alipozungumza na wananchi wa jimbo la Lushoto wilayani Lushoto, Tanga katika mkutano ya kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM Rais Dkt Magufuli, mgombea ubunge jimbo hilo Shabani Shekilindi na wagombea udiwani kwa tiketi ya CCM

Mheshimiwa Majaliwa ameitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa mradi wa maji VUGA (milioni 685), ujenzi wa mradi wa maji Kwalei (milioni 521) na ujenzi wa mradi wa maji Kasoli Mbuzii/Kwangwenda (milioni 262) ambayo ipo katika hatua za mwisho za utekelezaji wake.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa miradi ya barabara, Mheshimiwa Majaliwa amesema shilingi bilioni 1.225 zimetolewa na Serikali kupitia TARURA kwa ajili ya matengenezo ya kawaida, matengenezo ya sehemu korofi, muda maalum katika barabara hizo za Lushoto mjini, Boheloi-GareUbiri-MiegeoKizara-Kwemashai.

Mheshimiwa Majaliwa amezitaja barabara nyingine kuwa ni barabara za Dochi-GareMlalo-Ngwelo-MlolaMalibwi-MwekangaMajulai-Mlesa na barabara ya Mlola-Makanya kwa lengo la kufungua fursa za kiuchumi na kurahisisha usafirishaji wa watu na mizigo

Kuhusu uboreshwaji wa huduma za afya katika wilaya hiyo ya Lushoto Mheshimiwa Majaliwa amesema shilingi milioni 400 zimetolewa na Serikali kwa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambao tayari  umeanza.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amesema shilingi milioni 500 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Kangagai, ambazo zimetumika katika ujenzi wa wodi ya wazazi, maabara, nyumba ya kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi umekamilika na kituo kimeanza kutoa huduma.

“Shilingi milioni 500 zimetolewa kwa ujenzi wa kituo cha afya cha Mnazi. Fedha hizo zimetumika katika ujenzi wa wodi ya wazazi, maabara, nyumba ya kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi, ambao nao umekamilika na kituo kimeanza kutoa huduma kwa wananchi.”

Amesema kiasi kingine cha shilingi milioni 400 kimetolewa kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi, maabara, nyumba ya kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi katika kituo cha afya cha Mlola ambapo ujenzi wake umekamilika na kituo kimeanza kutoa huduma.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amesema kiasi kingine cha shilingi bilioni 2.3 zimetolewa kwa ajili ya uboreshaji wa zahanati ambapo zimetumika katika ujenzi wa zahanati tisa ambazo ni Kwamashai, Mpanga, Hambalawei, Nywelo, Mkunki, Tema, Masereka, Mlesa na Lukozi. Ujenzi umekamilishwa na Serikali, Halmashauri, wananchi pamoja na wadau wa maendeleo

Kuhusu ununuzi wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi, Mheshimiwa Majaliwa amesema kiasi cha shilingi bilioni 3.876 zimetolewa na Serikali katika kipindi cha miaka mitano sawa na wastani wa shilingi milioni 70Pia kituo cha Afya cha Mlalo kimepatiwa gari moja la kubebea wagonjwa.

IMETOLEWA:

IJUMAA, OKTOBA 9, 2020.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.