Habari za Punde

Zanzibar Yaadhimisha Siku ya Walimu Duniani.

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe akizungumza na Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali katika kuadhimisha Siku ya Walimu Duniani. hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara ya Elimu Mazizini Jijini Zanzibar.

Ndugu Walimu, Wanahabari na Wananchi wote kwa jumla

Asalam aleykum,

Awali ya yote hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutujaalia uhai, uzima na afya njema. Kama tunavyofahamu kuwa kila ifikapo tarehe 5 Oktoba ya kila mwaka tunasheherekea siku ya Walimu duniani. Zanzibar na Tanzania ikiwa ni sehemu ya Dunia hatuna budi kuungana na wenzetu kwa kusheherekea siku hii muhimu na adhimu kwetu. 
Kwa mwaka jana 2019 kwa Zanzibar Maadhimisho hayo yalifanyika kisiwani Pemba eneo la Uwanja wa Gombani na kwa mwaka huu yanafanyika katika Ukumbi wa Hospitali ya wagonjwa wa akili Kidonge Chekundu Zanzibar kwa kushirikiana na chama cha Walimu Zanzibar ZATU Pamoja na (OR) Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ.

Ndugu Wananchi

Mnamo  tarehe  05/10/1966, Umoja wa mataifa ulipitisha sheria mbili zinazoitwa
1. The ILO/UNESCO Recommendation Concerning the Status of Teachers, 1966.
2. The UNESCO Recommendations Concerning the Status of Higher Education Teaching Personnel, 1967.
Siku hii ni adhimu na pia ni muhimu kwetu kwa ustawi wa maendeleo ya elimu kwa kupitia kwa walimu, ambapo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya awamu ya saba inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein inathamini kwa dhati kabisa mchango na kazi kubwa ya walimu wanaoutoa sambamba na kuimarisha maslahi ya walimu Pamoja na kutatuwa changamoto zinazowakabili. Walimu ni kama watumishi wa Umma wengine ambao wana wajibu wao katika kutekeleza majukumu, haki, fursa na wanakabiliwa na changamoto mbali mbali. 

Katika awamu hii ya saba inayomalizika Serikali imefanikiwa kutatua changamoto za walimu zifuatazo:-

POSHO LA LIKIZO 
Wizara imelipa posho la likizo kwa walimu na wafanyaka la likizo. 

UZOEFU WA MIAKA 30 
Wizara imelipa wafanyakazi wenye uzoefu wa miaka 30 ya kazi (kwa agizo lilotolewa Febuari 2014 na kuanza kulipwa Novemba 2014.

MALIMBIKIZO YA WALIORUDI MASOMONI 
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali imelipa malimbikizo ya waliorudi masomoni ambapo mwaka 2018 imefanikiwa kulipa kiasi TSH 189,221,907. Pia katika uhakiki unaoendelea unatarajia kulipa awamu nyengine katika mwisho wa mwezi wa Oktoba 2020.

KUIMARISHWA KWA MASLAHI YA WALIMU
Katika awamu ya saba mbali na kuimarishwa maslahi ya walimu pia Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepandisha Mishahara ya Walimu mara tatu katika mwaka 2012, 2013 na 2017.

AJIRA YA WALIMU KWA KIPINDI CHA 2016 – 2020
NAM    MWAKA     UNGUJA         PEMBA    JUMLA
1    2016    51     37      88
2    2017    213  47     260
3    2018   723   278   1001
4    2019  238  213    451
5    2020   638  329    967
 JUMLA KUU  1863  904 2,767

Pia Serikali tayari ishaidhinisha kuajiriwa kwa walimu wote wanaojitolea kwa ngazi za maandalizi, msingi na sekondari, pamoja na walimu wa TUTU 868, kwa kweli haya ni mafanikio makubwa.

Ndugu Wananchi

Uimarishaji wa miundo mbinu ikiwemo skuli na Hub 
Kupitia mradi wa Zanzibar Improving Students Prospects (ZISP) Wizara imeweza kujenga Skuli ya Mwanakwerekwe na Wingwi pamoja na hub ishirini na mbili.

Pia kupitia mradi wa ZATEP Zanzibar Third Education Project Wizara imejenga Skuli 9 za ghorofa Unguja  na Pemba Skuli zenyewe ni:-

NA JINA LA SKULI   PAHALI
1. Skuli ya Sekondari ya Dk. Ali Mohamed Shein Rahaleo 
2. Skuli ya Sekondari ya Ali Hassan Mwinyi Bububu, 
3. Skuli ya Sekondari ya Dk. Salmin Amour Juma Chumbuni, 
4. Skuli ya Sekondari ya Abeid Aman Karume Kinuni 
5. Skuli ya Sekondari ya Aboud Jumbe Mwinyi Fuoni
6. Skuli ya Sekondari ya Dk. Aman Abeid Karume Micheweni, 
7. Skuli ya Sekondari ya Idrissa Abdulwakil Kizimbani, 
8. Skuli ya Sekondari ya Dk. Salim Ahmed Salim Wara/Chake Chake 
9. Skuli ya Sekondari ya Samia Suluhu Hassan Mwambe

Haya yote ni katika kuhakikisha mazingira mazuri ya kusomeshea yanapatikana kwa wanafunzi wetu na walimu kwa ujumla. Pia tunawashukuru jamii mbali mbali ambao wanaanza ujenzi wa madarasa na baadae yanamalizwa kwa kushirikiana na Wizara tunawapongeza sana na tunawaomba waendelee na moyo huo.

WATUMISHI WALIOTHIBITISHWA KAZI
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali katika kutekeleza matakwa ya kisheria imethibitisha kazi jumla ya Watumishi 2,974 katika mwaka 2011- 2019.

WATUMISHI WALIOPATA MAFUNZO
Wizara imewaruhusu watumishi 3,109 kwenda masomoni kwa mafunzo mafupi na ya muda mrefu ndani na nje ya nchi kwa viwango vya cheti, stashahada na shahada kwa kipindi cha mwaka 2013- 2019. (Mafupi 68 +2,976 marefu).

Ndugu Walimu

Nimalizie maelezo yangu machache lakini mazito kwa hadhi, heshima na siku ya leo nawapongeza walimu wote wa Zanzibar, Tanzania na Duniani kote. Pia tunakipongeza Chama cha Walimu cha Zanzibar ZATU kwa mashirikiano makubwa na Wizara na michango yao kwa kweli inatusaidia katika kufanikisha sekta ya Elimu nchini na tunawaomba tuzidi kushirikiane katika kulifikisha jahazi hili.

Mungu wabariki walimu 
Mungu ibariki Zanzibar, 
Mungu ibariki Tanzania.

Ahsanteni kwa kunisikiliza

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.