Habari za Punde

Makabidhiano ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar

WAZIRI Mstaaf ilioyokuwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu  akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Nyaraka za Kazi kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe Haroun Ali Suleiman (hayupo pichani) hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Mazizini Jijini Zanzibar leo 26/11/2020
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar  Mhe. Haroun Ali Suleiman akisaini hati ya makabidhiano  ya Nyaraka za Kazi baada ya kukabidhiwa na  Waziri Mstaaf iliokuwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Issa Haji Gavu (kulia kwake) hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Mazizini Jijini Zanzibar leo 
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akikabidhiwa Nyaraka za Kazi na Waziri Mstaaf iliyokuwa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu (kulia kwake) hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo
Mazizini Jijini Zanzibar leo 
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman akizungumza na kutowa shukrani kwa Waziri Mstaaf Mhe Issa Haji Gavu na Watendaji  wakati wa hafla ya makabidhiano ya Nyaraka za Kazi  zilizofanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Mazizini Jijini Zanzibar 
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na ( kulia kwake) Waziri Mstaaf Mhe.Issa Haji Gavu wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa makabidhiano ya Nyaraka za Kazi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Mazizini Jijini Zanzibar.
WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Zanzibar Mhe. Haroun Ali Suleiman na ( kulia kwake) Waziri Mstaaf Mhe.Issa Haji Gavu wakiitikia dua baada ya kumalizika kwa makabidhiano ya Nyaraka za Kazi, hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Wizara hiyo Mazizini Jijini Zanzibar
                                   

WAZIRI wa Nchi (OR) Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala bora, Haroun Ali Suleiman amewataka viongozi na watendaji wa Wizara hiyo kuendelea kufanyakazi kwa mashirikiano na uzalendo ili kutekeleza vyema majukumu yao.

Waziri Haroun ametowa wito huo leo Ofisini kwake Mazizini katika hafla ya makabidhiano kati  yake na Waziri mstaafu wa iliyokuwa (OR) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi ‘Gavu’, makabidhiano yaliozihusisha taasisi za Baraza la Mapinduzi pamoja na Ofisi ya Usalama wa Serikali (GSO).

Amesema maagizo yaliotolewa na Rais wa Zanzibar kwa Mawaziri wakati wa zoezi la kuapishwa  yana lengo la kuwataka watendaji wote wa serikali kutekeleza vyema majukumu katika sekta zao  ili kuleta tija katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aliwataka kila mmoja kuwajibika kwa nafasi yake, huku akionya kutofadhaika katika utekelezaji  wa majukumu yao kutokana na mchakato wa uteuzi wa watendaji wa Serikali unaoendelea.

Alisema ni jambo la faraja kwa hatua ya Rais Dk. Mwinyi kuzipeleka taasisi hizo katika Wizara hiyo .

Nae, Waziri Mstaafu Wizara ya Nchi (OR) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi ‘Gavu’ aliwashukuru viongozi na watendaji wote wa iliyokuwa Wizara hiyo kwa kufanyakazi kwa mashirikiano na upendo na kutaka kuhamishia juhudi hizo katika Wizara hiyo mpya.

Alisema ana imani kubwa kuwa yale yote mazuri waliyomfanyia na kufanikisha utekelezaji mzuri wa majukumu yake watayaendeleza chini ya Uongozi wa Waziri Haroun.

Aidha, alimtakia Waziri huyo utekelezaji mwema wa majukumu ya kazi zake  na kubainisha imani aliyonayo katika kuendeleza na kukamilisha mchakato wa sheria ya GSO aliyoiasisi.

Katika hafla hiyo Waziri Gavu alimkabidhi Waziri Haroun nyaraka mbili kutoka taasisi za Baraza la Mapinduzi na Ofisi ya Usalama wa Serikali (GSO) ambamo ndani yake kumebainishwa Bajeti, changamoto na mafanikio ya ofisi hizo.

Wakati huo huo, Waziri mstaafu wa iliyokuwa (OR) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi ‘Gavu’ alikabidhi taasisi mbali mbali kutoka  iliyokuwa Wizara hiyo kwa Waziri wa Nchi (OR) Uchumi, Uwekezaji  Mudrik Ramadhan Soraga.

Taasisi hizo ni pamoja na Ofisi ya faragha, Habari na Mawasiliano Ikulu, Idara ya Mipango; sera na Utafiti , Diaspora pamoja na Ofisi Kuu Pemba. 

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri Soraga aliahidi kushirikiana na kufanyakazi kwa karibu na watendaji wote wa Wizara hiyo, huku  akisisitiza umuhimu wa wafanyakazi hao kufanyakazi kwa pamoja (team work).

Alisema suala la mawasiliano ili kufikia maamuzi sahihi kiutendaji ni muhimu katika mustakbali mwema wa nchi.

Aidha, alibainisha matarajio yake kwa watendaji kuzingatia miiko ya utumishi wa umma kwa kulinda siri na kuepuka kutoa taarifa pamoja na kuhakikisha ofisi hiyo inaondokana na matukio ya ajabu na hivyo kuharibu sura ya Ofisi hiyo.

Mapema, Waziri mstaafu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Ussi ‘Gavu alimpongeza Waziri Mudrik kwa kuteuliwa kushika wadhifa huo na kubainisha imani kubwa aliyonayo kutokana na nguvu na uwezo mkubwa alionao katika kusimamia Wizara hiyo.

Alimuomba kuendelea na mchakato wa uanzishaji wa sera ya Diaspora, akibainisha mabadiliko ya kisheria ni muhimu katika kuwapatia fursa wana Diaspora  kutekeleza mambo yenye faida kwa Taifa.

Aidha, Katibu wa Rais wa Zanzibar Suleiman Ahmeid Saleh alisisitiza umuhimu wa watendaji kufanyakazi kwa bidi, weledi na uaminifu ili kufanikisha azma ya Rais ya kuipatia Zanzibar mafanikio.

Katika hafla hiyo Waziri mstaafu Gavu alimkabidhi Waziri Soraga nyaraka mbali mbali za Ofisi hizo zinazohusisha Muundo, Bajeti pamoja na Programu mbali mbali zikielezea matatizo na mafanikio yake.     

 Abdi Shamna, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777476982. Fax: 024 2231822 

 E-mail: abdya062@gmail.com


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.