Habari za Punde

Hospitali ya Uhuru Yaunganishwa na Mkongo wa Taifa wa mawasiliano

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, (iliyokuwa Sekta ya Mawasiliano), Dkt Jim Yonazi akizungumza timu aliyoambatana nayo katika kukagua uingizaji wa fibre za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, vyumba vitakavyowekwa mifumo ya TEHAMA, pamoja na upatikanaji wa mawasiliano ya simu za mkononi na data katika Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino jijini Dodoma, jana. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, (iliyokuwa Sekta ya Mawasiliano), Dkt Jim Yonazi akikagua uingizaji wa fibre za Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino jijini Dodoma, jana. 


Na Faraja Mpina(WMTH)

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari iliyokuwa Sekta ya Mawasiliano, Dkt Jim Yonazi ametembelea na kukagua hatua iliyofikiwa ya  ujenzi wa miundombinu ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika hospitali ya Uhuru inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, jijini Dodoma

Dkt Yonazi amekagua Ujenzi wa wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, vyumba maalumu ambavyo mifumo ya TEHAMA itafungwa na kuunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano pamoja na  upatikanaji wa huduma za mawasiliano ya sauti na data ikiwemo mitandao ya simu za mkononi

Dkt. Yonazi amesema kuwa lengo la kufanya ukaguzi huo ni kuhakikisha kuwa huduma bora za mawasiliano katika hospitali hiyo zinapatikana na zinazingatia  matumizi ya kisasa ya TEHAMA

“Jukumu letu la msingi ni kuwezesha sekta mbalimbali kutumia TEHAMA ikiwemo Sekta ya Afya, lengo ni kuhakikisha Sekta ya Afya inatumia TEHAMA katika kutoa huduma zake kwa wananchi ikiwemo elimu ya afya kwa njia ya mtandao”, amesisitiza Dkt Yonazi

Naye Meneja wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Mkoa wa Dodoma, Simon Marwa amesema kuwa ujenzi wa miundombinu hiyo umefikia kiwango cha asilimia 60 na utakamilika na kuwa tayari kutumika mara hospitali hiyo itakapoanza kutoa huduma.

Katika hatua nyingine Marwa amesema kuwa TTCL inajipanga kutekeleza agizo la Dkt. Yonazi la kuhakikisha huduma za intaneti zinapatikana kwa wananchi watakaofika katika hospitali hiyo pamoja huduma za kuweka na kutoa pesa mtandaoni kwa kutumia T-Pesa

Aidha, Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto wa Wilaya ya Chamwino, Neema Mlula amesema kuwa kuwekwa kwa miundombinu hiyo na mifumo ya TEHAMA katika hospitali hiyo kutawezesha utoaji wa huduma za afya, kukusanya takwimu na kuhifadhi kumbukumbu za wagonjwa

Ameongeza kuwa, mifumo ya TEHAMA itaunganishwa kwenye  vitengo nane vya hospitali hiyo ili kufanikisha utoaji wa huduma bora na kwa wakati, huku akivitaja vitengo hivyo kuwa ni wagonjwa wa nje, idara ya mionzi, maabara, kitengo cha dawa,idara ya macho, idara ya afya ya kinywa na meno, idara ya utawala na idara ya afya ya uzazi na mtoto.

ImetolewanaKitengo cha MawasilianoSerikalini

WizarayaMawasilianonaTeknolojiaya Habari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.