Habari za Punde

Rais Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Amefanya Ziara ya Kukagua Mradi wa ZUSP Kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar Hadi Kilimani Kwa Kutembea kwa Miguu leo Asubuhi.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe, Jamal Kassim Ali alipowasili katika eneo barabara ya Uwanja wa Ndege kuaza ziara yake kutembelea Mradi wa Huduma za Jamii Mijini ZUSP kuangalia maendeleo ya ujenzi wa mtaro wa maji machafu pembezoni mwa barabara hiyo ikiwa chini ya mradi huo na uwekaji wa taa za barabarani. akiwa katika ziara yake hiyo na kutembea kuazia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume hadi Kilimani kuangalia utekelezaji wa wake.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mratibu wa Mradi wa Huduma za Jamii Mijini ZUSP Ndg. Makame Ali Makame akitowa maelezo wakati wa ukaguzi Mradi huo wa Ujenzi wa Mtaro wa maji machafu na uwekaji wa taa katika barabara hiyo, akiwa katika ziara yake kutembelea Mradi huo leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapiduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitowa maelekezo kwa Mratibu wa Mradi wa Huduma za Jamii Mijini ZUSPO Ndg. Makame Ali Makame  mwenye maiki  kutoridhika ma utekeleza wa mradi huo na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.Mhe Idrisa Mustafa Kitwana.
Wapiga picha za Video wakiwa makini kuchukua matukio wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza wakati wa ziara yake hiyo katika eneo la barabara ya kiembesamaki Jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitowa maelekezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Ndg. Mustafa Aboud Jumbe wakati wa ziara yake kutembelea Mradi wa Huduma za Jamii Mijini ZUSP, unaotekelezwa Unguja na Pemba na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja. Mhe Idrisa Mustafa Kitwana. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akikagua Mradi wa Huduma za Jamii Mijini ZUSP akiwa katika ziara yake hiyo ilioanzia katika eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa kutembea hadi Kilimani Jijini Zanzibar kuangalia ujenzi wa mtaro wa maji machafu na (kulia kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Maryam Mwinyi na Spika wa Baraza la Wawakilishi Mhe. Zuberi Ali Mauli na (kushoto kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe. Idrisa Mustafa Kitwana na Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Mhe. Rahma Kassim Ali.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa mtaro huo ulioko kando ya barabara ya kiembesamaki Jijini Zanzibar kama wanavyoonekana pichani wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akitowa maelekezo kwa Mkadarasi wa Kampuni ya STC Construction Ndg.Allan Makame (kushoto kwa Rais) aliyeweka taa katika barabara ya kiembesamaki na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Mhe. Jamal Kassim Ali,  wakati wa ziara yake kutembelea mradi wa ZUSP aliyoifanya leo jijini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kutowa maellekezo kwa Uongozi wa Wizara ya Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango kukamilisha Mradi huo kwa wakati uliowekwa , baada ya kumaliza ziara yake katika eneo la Kilimani Jijini Zanzibar leo 9/12/2020.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.