Habari za Punde

Naibu Mrajis wa Vyama vya Ushirika Malunde Awataka Wafugaji Kubadilika na Kuacha Ufugaji wa Mazoea.

 

Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Charles Malunde akisistiza jambo wakati wa mkutano huo kulia ni Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Tanga, Jackline Senzighe


Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Charles Malunde akisistiza jambo wakati wa mkutano huo kulia ni Mrajis Msaidizi wa Vyama vya Ushirika mkoa wa Tanga, Jackline Senzighe

Sehemu ya wadau wakiwemo viongozi wa chama cha ushirika na ufugaji ambavyo vimeunda chama kikuu cha ushirika wa maziwa Tanga wakimsikiliza kwa umakini Naibu Mrajisi wa vyama ushirika kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika
Mmoja wa wanaushirika akiuliza swali katika mkutano huo

 

Naibu Mrajisi wa Vyama vya Ushirika nchini kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika,Charles Malunde amewataka wafugaji kubadilikana watoke kwenye ufugaji wa mazoezi badala yake wafuge kisasa ili waweze kupata manufaa makubwa yanayotokana na eneo hilo.

Malunde aliyasema hayo mjini Tanga wakati alipokutana na viongozi wa chama cha ushirika na ufugaji ambavyo vimeunda chama kikuu cha ushirika wa maziwa Tanga wakati wa ziara yake.

Alisema wafugaji hao wanapaswa kubadilika kutokana na alichobaina kwenye ziara yake kuna wafugaji kwa ng’ombe wanapata lita nne kwa sababu ya matunzo mabaya na yanapokuwa matunzo mazuri yule ngombe anabadilika anatoka kwenye lita nne hadi ishirini.

Malunde alisema kwa hiyo ukiangalia wakati fulani mfugaji anaangalia anachokipata kutokana na kile alichowekeza lakini kumbe tatizo linakuwa kutokana na matunzo mabaya ndio maana uzalishaji wa maziwa umekuwa kidogo.

“Kuna mambo tumejadilia hapa ikiwemo suala la bei..bei wakati wote imeonekana sio rafiki kwa mfugaji lakini ahadi ambayo nimeitoa pamoja na hili ambalo linaweza kuangaliwa lakini wafugaji wenyewe waone kuna haja ya kuangalia namna ya utunzaji bora kuwalisha vizuri mifugo ili waweze kupata maziwa mengi”Alisema

Hata hivyo alisema suala jingine namna ya kupata mitamba bora bila kuingia kwenye mikopo huku akitolea mfano kwa wafugaji hao kwamba wakiwekeza kila siku lita tano za maziwa wanazotoa baada ya mwaka mmoja zitakuwa zimetosheleza kununua mtamba mmoja.

Aliongeza kwa hiyo kwa sababu ya serikali na tume ya maendeleo ya Ushirika wamehamasisha kuundwa sacoos mahali penye amcos hivyo ametoa wito waendelee kuliangalia hilo kuna uwezekano mkubwa wa kupata mitamba kwa kudunduliza kwao bila kuhitaji taratibu za kupata mikopo.

Alisema kutokana na kwamba inachukua muda mrefu zaidi ya mwaka mmoja mpaka miaka miwili kama ni hivyo kupitia kwenye hizo taratibu zao kuna uwezekano wakaanzisha huo utaratibu mitamba inaweza kupatikana ndani ya miezi sita wakati atakapokuwa akiendelea kudunduliza maziwa yake huo ni mfano.

Katika hatua nyengine aligusia suala la wafugaji ambao wanaondoka na kwenda kuuzia sehemu nyengine ambapo alitoa onyo vyama vya ushirika kuacha kufanya hivyo mara moja.

“Kuna chama cha ushirika ambacho kimeonekana kukusanya maziwa ya mfugaji kwa bei fulani halafu kinakwenda kuuza sehemu nyengine viongozi ambao wameonekana kufanya hivyo ameagiza wale maafisa ushirika sehemu walipo wawachukulie hatua ikiwemo kuwaondoa kwenye nafasi zao”Alisema

Alisema wachukua maamuzi hayo ili kusudi ikawe fundisho kwa wenzao kwa sababu lengo lilikuwa wakikisanya wanaunganisha nguvu ya pamoja lakini hao wanachukua maziwa na kwenda kuuza maeneo mengine pembeni hiyo ni hujumu.

Malunde alisema kwa namna hiyo na kwa kufanya hivyo wanausaliti ushirika ulioundwa na wao kama wanausimamia wanawaona hawafai na kwa sababu kama bado wapo viongozi ambao wanawasaidia hao ndio wanawahitaji warudi na kubadilishwa viongozi wengine ambao wanaweza kuusimamia ushirika.

Awali wakizungumza katika mkutano huo Mwanahawa Hiza kutoka Chama cha Ushirika cha Uviwaki Pingoni Jijini Tanga alisema kwamba wao changamoto yao ni kipindi cha ukame maziwa yanakuwa madogo na hayapatikani.

Alisema lakini kipindi cha mvua wakati wa kuchukua maziwa kuyapeleka mjini kuna maeneo mengine korofi na hivyo kuwa na changamoto.

Aidha alisema pia bei ya maziwa sio nzuri maziwa wanauza lita sh.820 wakiwaambia waongeze bei wanasema bei ni hiyo hiyo huku malisho ya ngombe yakiendelea kuwa ghali.

“Kipindi cha mvua kutoa Maziwa eneo la Pingoni Kata ya Pongwe hadi mjini Tanga kuna maeneo magari yanakwamba na hivyo kufanya ucheleweshwaji wa fedha”Alisema

Aliomba serikali iangalie suala la bei kutokana na kwamba wafugaji wanateseka waweze bei ya uwiano kwa pamoja na haiwezi kukaa hivyo hivyo miaka yote.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.