Habari za Punde

Taasisi ya Elimu Zanzibar kupitia mtaala wa Elimu ya maandalizi na msingi

 Na Maulid Yussuf WEMA


Taasisi ya Elimu Zanzibar imesema itaendelea na juhudi zake katika kuhakikisha inapitia vyema   ili Taifa lipate Elimu bora.  

Akizungumza wakati akifungua warsha ya siku moja  ya kupitia na kuchangia mawanda ya mtaala wa Wanafunzi wa maandalizi na msingi Kwa  maafisa wa Taasisi ya Elimu Zanzibar ,Mkurugenzi wa Taasisi hiyo mwalimu  Suleiman  Yahya  Ame amesema suala la mitaala katika kila nchi ni muhimu sana kwa maendeleo ya Taifa lake.


Amewataka watendaji wa Taasisi hiyo kuhakikisha wanafuatilia kwa makini muendelezo mzima wa mapitio ya mtaala ili kuweza kutambua hatua zilizofikia na kuweza kuielimisha jamii inayowazunguka kwa lengo la kuwatoa hofu kuhusu mtaala uliopo.

Mwalimu Suleiman amewataka watendaji hao kuitumia vizuri  nafasi hiyo kwa kuchangia na kutoa maoni yao ili kuleta maendeleo katika nchi .

Pia amewashauri wazazi na jamii kwa ujumla kuendelea kutoa maoni yao juu ya masuala ya marekebisho ya mtaala kadri watakavyohitajika ili kuweza kulisaidia Taifa kupata mtaala ulio bora kwa maendeleo ya watoto wao.

Nae  Meneja Idara ya Mitaala na vifaa kutoka Taasisi ya Elimu  Zanziar, Mwalimu Abdullah Mohammed Mussa  amesema watawasilisha Mawanda ya Maandalizi katika masomo sita ya 
mawanda ambayo yapo katika Mfumo wa Maudhui.

Hivyo amewaomba watedaji hao kuyapitia na kuyaelewa mawanda hayo ya Mitaala pamoja  na kushauri zaidi yale ambayo wanaona yanafaa kutumia katika mtaala utakapokamilika.

Pia ameeleza kuwa mtaala mpya unazingatia sana umahiri wa mtoto, hivyo amewataka pia kuangalia ujuzi ambao umewekwa katika Mawanda kwa  upande wa kusoma , kuandika pamoja na maswala ya ubunifu ili uweze kumsaidia mtoto na kuhakikisha anapata Elimu bora.


Akiwasilisha mawanda ya mtaala huo, Kaimu Mkuu wa Divisisheni ya ukuzaji Mitaala ya Elimu ya Maandalizi na Msingi Mwalimu Patima Kheri Koba amesema Katika mtaala huo utawawezesha watoto kuweza kujifunza mambo mbali mbali pamoja na kupata ubunifu utakaokumkuza mtoto kiakili.

Pia ameleza kuwa kuna Maudhui kumi katika maeneo ya kujifunza kwenye mtaala huo ikiwemo sanaa za Ubunifu , Sanaa za michezo , Sanaa za Lugha na Sanaa nyengine.


Akitoa Neno la shukran  kwa niaba ya maafisa wa Taasisi ya Elimu Zanzibar, Bi Asha Soud  Nassor  Ambae ni Mratibu wa Taasisi  ya Elimu Pemba amemshukuru Mkurugenzi wa  Taasisi ya Elimu kwa muongozo alioutowa kuhusu  mtaala mpya wa Elimu, hivyo wanaahidi kutekeleza ili kuleta maendeleo katika nchi yetu .

Warsha hiyo ya siku moja imewashirikisha watendaji wa Taasisi ya Elimu wa Unguja na Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.