Habari za Punde

UZINDUZI WA "WANAWAKE LAKI MOJA" MKOANI MWANZA DESEMBA 5,2020

 

 
WANAWAKE laki moja ni Asasi iliyoanzishwa kwa kufuata sheria  na taratibu za Nchi mnamo mwezi wa Kwanza 2020.

Lengo lake kuu ni Kuunganisha  Wanawake wote Nchini Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Umaskini.

Mpaka sasa mtandao huu una wanachama katika Mikoa 17 Nchi nzima na kila Mkoa una uongozi ambao una Mwenyekiti, Katibu na Mwekahazina.

Mnamo tarehe 5/12/2020 Asasi ina kwenda kuzinduliwa ndani ya Ukumbi wa Banki kuu (BOT) Mkoani Mwanza kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni kwa kiingilio cha Shilingi elfu ishirini tu.

Kwa atakayetaka kushiriki na kuwa mwanachama anaweza ku wasiliana kwa njia ya WhatsApp kwa kutuma ujumbe kwa Katibu wa Mtandao Bi Josephine Ngoda kwa namba..0620765411

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.