Habari za Punde

Hakuna mgao wa FIFA kwa Zanzibar : Karia

 NA MWAJUMA JUMA

SHIRIKISHO la Soka Tanzania TFF limesema hakuna mgao wa FIFA kwa Zanzibar na fedha ambayo unakuja ni kwa ajili ya shughuli za mpira wa miguu Tanzania.

Kauli hiyo ilitolewa na Rais wa TFF Wares Karia alipozungumza na waandishi wa habari ambao walitaka kujua jinsi ya mgao huo kwa Zanzibar.

Alisema kuwa fedha ambazo zintumwa sio za mgao wala hazigawiwi kwa sababu zinakuja kwa shughuli maalumu.

Hivyo alifahamisha kwamba watakapogawa inamaana kuna.shughuli zao nyingi zitasita ikiwemo timu za taifa nazo kukosa kushiriki.

"Sisi Kama Shirikisho tuna timu zetunza Taifa na hatuna ruzuku yoyote kutoka serikalini na tunatayarisha semina za waamuzi, makocha, Mafunzo ya Utawala na tunashughulikia timu zetu Taifa na kushiriki mashindano yote yanayostahiki timu zetu za taifa  na ni peke yake Shirikisho ambalo halina ruzuku serikalini ", alisema.

Hata hivyo alisema kwamba kwa sasa timu ya Taifa ipo katika mashindano na U-20 wapo Arusha na TD anazunguka mikoani na.gharama zote wanatoa wao.

Aidha alisema kuwa iwapo zinapokuja timu za kugawa kama ambavyo katika Kipindi cha maradhi ya corona waliweza kusaidia na Zanzibar ikiwemo kuwapa fedha za kusaidia ligi yao.

"Lakini suala la kusema fedha itakatwa pasu wala hamna na hatuwezi kufanya, ni jambo ambalo litatusababishia sisi tushindwe kupata fedha na pia shughuli zetu zote za maendeleo zitasimama", alisema.

Alieleza kwamba wanachokihangaikia wao kwa sasa ni kuona kwamba kunakuwepo na rekognation wa angalau kuweze kuchezwa mpira na kuna watu zaidi ya milioni mbili lakini kuna watu wanacheza mpira 50,000 tu lakini wanapata fedha kama ambayo wanapata wao.

Hivyo wanataka kujenga hoja angalau zile fedha ziweze kupatikana kwa Zanzibar.

Alisema kuwa na hilo wanaenda kujaribu kulizungumzia kwa taratibu kwani watakapokwenda kiubabe hawatoweza kufanikiwa.

Kuhusu Zanzibar kuingizwa CAF na baadae kutolewa hapo alisema huenda kuna suala la kisheria halikufuatwa hivyo wanataka wakae kuangalia ni utaratibu gani uliotumika kwa vile wakiwa wanachama wanaweza kufaidika na kile kiwango kinachotolewa na CAF.

"Kwa mtazamo wa kisheria kunaonekana kuna suala la kisheria halikufatwa kwa hivyo tunataka tuangalie kwa jinsi gani walipunguzwa na mkutano mkuu na kutolewa kwa utaratibu ambao haueleweki   lakini wakiwa wanachama wanaweze kupata angalau kinachotolewa na CAF", alisema.

Hivyo alisema kuwa kwa suala hilo la mgao wa FIFA kupewa wao mtu asifikirie kabisa Kama kuna siku Itaweza kugawiwa.

Kuhusu Zanzibar kuwa wanachama wa FIFA alisema ni suala ambalo amekuwa akilifanya kila siku lakini ni jambo la kuangaliwa je Zanzibar nako kumetulia kwenye chama cha mpira.

"Sasa hivi tunapozungumza hapa nimepata habari ambazo zimenisikitisha  sana kweli na kama ningalijuwa mapema nisingeleta Mafunzo hapa kwa sababu mimi nataka kujenga mpira na hayo mambo ya kufukuzana yameshapitwa na wakati na.sasa hivi kuleta maendeleo", alisema.

Alisema mpira ni jambo ambalo linaleta mahusiano ya karibu na kuhoji "kwanini wanasiasa wameungana, kwanini tusiungane tukafanya jambo ambalo linaweza kutuleta pamoja".
Kwa upande wake rais wa Shirikisho Zanzibar ZFF  Seif Kombo alisema Karia amejibu hivyo kwa sababu mazungumzo yao na walivyokubaliana kuwa pesa ya FIFA na CAF inakuja kwa bajeti maalumu ambayo hawawezi kuigawa, isipokuwa suala la kujiuliza ni kwamba kwanini miradi yote ifanyike Tanzania Bara.

“Hoja ya kugawana pesa sawa imekubalika lakini kwanini huo uwanja wasijenge na Zanzibar na kwanini kila kitu kifanyike bara”, alihoji Seif.

Alieleza kuwa tayari walishakaa kikao na wenzao wa TFF na wakakubaliana ili yaondoke  masuala haya kitu cha mwanzo na cha msingi ni kuhakikisha kwamba wanapata uwanachama wa CAF na FIFA.

Alisema kuwa hatua hiyo itaisaidia Zanzibar kufikia maendeleo ya haraka kwa sababu kiasi hicho cha fedha watakachokipata ni za watu kidogo ikilinganishwa na wao.

Aidha alisema kuwa katika kikao hicho TFF waliweza kuwapa  utaratibu ulivyo kwamba nchi zote duniani ambazo ni wanachama wa FIFA wanapewa dola milioni moja au tano kwa mfano wakajenge kiwanja cha mpira chenye viwango vya FIFA sasa iwapo watazigawa kwa ZFF kudai fedha hizo hawatoweza kukamilisha miradi yao na itawaletea matatizo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.