Habari za Punde

Rais Hussein Mwinyi alifungua Jengo jipya la Ofisi za ZSSF Tibirizi “Hifadhi Building” Chakechake Pemba

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikata utepe kulifungua Jengo jipya la Ofisi za ZSSF Tibirizi “Hifadhi Building” Chakechake Pemba na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Maalim Seif Sharif Hamad, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mjenzi wa Jengo la Ofisi za ZSSF Hifadhi Building lililoko katika eneo la Tibirinzi Chakechake Pemba Mkurugenzi wa Kampuni ya Quality Building Contractor Ndg. Khamis Ali Shaib akitowa maelezo ya ujenzi huo wakati wa ufunguzi uliofanyika leo 5/1/2021 na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe.Maalim Seif Sharif Hamad na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi na (kushoto kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, wakimsikiliza Meneja Mipango Uwekezaji na Utafiti wa ZSSF Ndg. Abdulazizi Ibrahim Iddi, akitowa maelezo wakati wa kutembelea moja ya Nyumba ilioko katika jengo la Ofisi za ZSSF “Hifadhi Building “ baada ya kulifunga leo 5/1/2021 ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akiondoka katika viwanja vya Jengo Jipya la Ofisi za ZSSF LA Hifadhi Building, baada ya kulifungua ikiwa ni shamrashamra za sherehe za Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar na (kulia kwa Rais) Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe. Jamal Kassim Ali.
WANANCHI wa Chakechake Pemba wakifuatiliac hafla ya ufunguzi wa Jengo jipya la Ofisi za ZSSF la Hifadhi Building lililoko katika eneo la Tibirinzi, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
BAADHI ya Viongozi wa Serikali na Wananchi wakifuatilia hutuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akiwahutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Ofisi za ZSSF Tibirinzi Chakechake Pemba ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
MKALIMALI wa lugha za Alama Bi. Asha Issa Mohammed akitowa maelezo kwa vitendo kwa baadhi ya Wananchi wenye ulemavu wa kutokusikia, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika viwanja vya Tibirinzi Chakechake Pemba.

WAZIRI wa Nchi Afisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Mhe.Jamal Kassim Ali akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi,kuzungumza na Wananchi wa Pemba wakati wa hafla ua ufunguzi wa Ofisi za ZSSF Tibirinzi 
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa hafla ufunguzi wa Jengo jipya la Ofisi za ZSSF Hifadhi Building lililopo katika eneo la Tibirinzi Chakechake Pemba, ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea Miaka 57 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
VIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Jengo jipya la Ofisi za ZSSF la Hifadhi Building Tibirinzi, wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akihutubia katika hafla hiyi iliofanyika katika kiwanja cha Watoto Tibirinzi Chakechake Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.