Habari za Punde

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi Azungumza naJumuiya ya Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni Binafsi Nchini Tanzania Ikulu.

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi akizungumza na Ujumbe wa Jumuiya ya Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni Binafsi Tanzania wakati wa mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 22-1-2021, walipofika kwa mazungumzo na Rais wa Zanzibar.

Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni Binafsi Tanzania wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) akizungumza wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni Binafsi Nchini Tanzania Bw. Dino Stengel akizungumza wakati wa Mkutano wao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa mkutano wao uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo 22-1-2021. 
Baadhi ya Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni Binafsi Nchini Tanzania wakifuatilia mkutano wao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar leo.22-1-2021.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisisitiza jambo wakati wa mkutano wake na Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni Binafsi Nchini Tanzania walipofika Ikulu Zanzibar kwa mazungumzo yaliofanyika leo 22-1-2021. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ADVENT Ndg. Dhruv Jog akizungumza wakati wa mkutano huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi ulifanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Maendeleo ya Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Ndg, Shariff Ali Shariff akijibu  maswali yaliouliwa wakati wa mkutano wa Jumuiya ya Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni Binafsiu Nchini Tanzania wakati wa mkutano wao na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HANSPAUL Ndg. Satbir Singh Hanspaul akizungumza wakati wa mkutano huo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Hussein Ali Mwinyi ulifanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa picha ikionesha mandhari ya Mji Mkongwe wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni Binafsi Tanzania.Bw.Dino Stengel, baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuagana na Wajumbe wa Jumuiya ya Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni Binafsi Tanzania baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi alikutana na Jumuiya ya Wakurugenzi Watendaji wa Makampuni binafsi ya Tanzania ambapo katika maelezo yake aliwaeleza azma ya Serikali ya Awamu ya Nane ya kuimarisha uchumi wa buluu pamoja na kupitia sekta za biashara, uwekezaji na  utalii.

Rais Dk. Mwinyi aliwaeleza wakuu hao wa Kampuni hiyo kwamba Serikali tayari imeshawekea mazingira mazuri ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na kuiimarisha Mamlaka ya ZIPA ili iweze kutoa huduma vizuri.

Nao Wakurugenzi hao Watendaji walieleza azma yao ya kuja kuekeza Zanzibar na kueleza walivyovutiwa na jitihada za Serikali chini ya uongozi wa Rais Dk. Mwinyi.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.