Habari za Punde

DKT CHAULA AWAKUTANISHA WATAALAMU WA MAWASILIANO NA TEHAMA KUJADILI MASUALA YANAYOHUSU MIUNDOMBINU YA KIMKAKATI YA MAWASILIANO

 

Na Faraja Mpina - WMTH

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainab Chaula amefungua kikao cha wadau wataalamu wa mawasiliano na TEHAMA kilichoitishwa na Wizara hiyo ili kujadili, kutoa maoni na ushauri juu ya namna bora ya kuboresha miundombinu ya kimkakati inayowezesha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano nchini.

Akizungumza katika kikao cha wataalamu hao kilichofanyi katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, Dkt chaula amewaambia wataalamu hao kuhakikisha wanaibua hoja zenye tija zitakazoleta msingi wa kuboresha na kulinda miundombinu hiyo itakayo saidia kuinua uchumi wa nchi na kuongeza mchango wa Wizara kwenye Pato la Taifa.

Ameongeza kuwa miundombinu hiyo inawezesha upatikanaji wa fursa mbali mbali ikiwemo biashara mtandao na upatikanaji wa huduma mbali mbali za kijamii kupitia mifumo ya TEHAMA huku akizitaja changamoto zinazoambatana na fursa hizo ni pamoja na wizi, uhalifu wa njia ya mtandao na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii.

“Tumewaita hapa wadau wataalamu wa mawasiliano na TEHAMA kutoka katika taasisi za Serikali na binafsi ili watoe maoni na ushauri kwa Wizara ili kuisaidia Wizara pindi inapotengeneza sheria, kanuni, mifumo na miongozo mbali mbali iwe na majumuisho na michango ya wadau wataalamu katika maeneo hayo”, Dkt.Chaula

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt Jim Yonazi ametoa rai kwa wataalamu hao kutumia utaalamu wao wote kuhakikisha wanatoa mchango ambao utaifanya nchi ya Tanzania kuwa kinara wa miundombinu bora ya mawasiliano kuanzia katika ujenzi, uendelezaji na ulinzi wa miundombinu hiyo.

Aidha, ametoa maagizo kwa kikao hicho kuainisha wadau muhimu waliosahaulika kupewa mualiko wa kikao hicho ili waweze kushiriki katika kikao kijacho kwa sababu ni muhimu sana kupata mchango wa wataalamu wote muhimu ili kuboresha miundombinu ya mawasiliano nchini.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa TEHAMA wa Wizara hiyo, Mulembwa Munaku amesema miundombinu ya kimkakati ni ile inayosaidia matumizi ya TEHAMA nchini ambayo ikiharibika au kuhujumiwainaathiriuchumiwanchi, usalamanahuduma za kijamii.

AmesemakuwakikaohichokinajadilivigezovyamiundombinuhiyoiliWizarakuwekautaratibuwakuiendeleza, kuilindanakuiepushanahujumambalimbalizinazofanyikakatikamiundombinuhiyo.

NayeNkundweMosagaMhadhirikutokaTaasisiyaTeknolojia Dar es Salaam ambayenimtaalamuwa TEHAMA amesemakuwamifumoyaTEHAMA ndioinayobebamaononamuelekeowanchikwakuchangiaukuajiwauchuminakutengenezaajirakwawananchi

MenejawamiundombinuyamawasilianokutokaKampuniyasimuya Vodacom Michael BujagaameishukuruWizarakuandaakikaohichoilikutafutaufumbuzikwenyemasualayamiundombinuhiyoinayonufaishataasisi za mawasiliano, watumiajiwahuduma za mawasilianonanchikwaujumla.

ImetolewanaKitengo cha MawasilianoSerikalini

WizarayaMawasilianonaTeknolojiaya Habari

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.